Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (katikati), akikata utepe kuashiria
kuzindua rasmi Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
Mzunguko wa Pili katika Mkoa wa Mtwara. Uzinduzi huo ulifanyika katika
kijiji cha Namtumbuka, Mtwara Vijijini, Juni 19, 2021.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Wakili
Julius Kalolo akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi
Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili
katika Mkoa wa Mtwara. Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha
Namtumbuka, Mtwara Vijijini, Juni 19, 2021.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifurahi pamoja na
vijana wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi Mtwara Vijijini, baada
ya uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya
Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa wa Mtwara. Uzinduzi huo ulifanyika
katika kijiji cha Namtumbuka, Mtwara Vijijini, Juni 19, 2021. Wanafunzi
hao walisema umeme utawawezesha kuongeza ufaulu katika masomo yao.
Mkurugenzi
wa Huduma za Ufundi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi
Jones Olotu akizungumza na wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa
Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa
Pili katika Mkoa wa Mtwara. Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha
Namtumbuka, Mtwara Vijijini, Juni 19, 2021.
Sehemu
ya umati wa wananchi wakishangilia wakati wakimsikiliza Waziri wa
Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao
wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini
Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa wa Mtwara. Uzinduzi huo
ulifanyika katika kijiji cha Namtumbuka, Mtwara Vijijini, Juni 19, 2021.
Wafanyakazi
wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakimpongeza Zairu Bakari,
mwanafunzi wa Darasa la Pili, Shule ya Msingi Namtumbuka, ambaye
alishiriki pamoja na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa
Nishati Dkt. Medard Kalemani kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili
katika Mkoa wa Mtwara. Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha
Namtumbuka, Mtwara Vijijini, Juni 19, 2021.
Mjumbe
wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REB), Oswald Urasa akiwasalimu
wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza
Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa wa Mtwara.
Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Namtumbuka, Mtwara Vijijini,
Juni 19, 2021.
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa tatu-kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mtwara, Wakala wa Nishati
Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wizara hiyo
alipowasili mkoani humo kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa
Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa wa
Mtwara. Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Namtumbuka, Mtwara
Vijijini, Juni 19, 2021.
…………………………………………………………………………………………………
Na Veronica Simba – REA
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amezindua Mradi Kabambe wa Kusambaza
Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa wa Mtwara
unaolenga kufikisha umeme katika vijiji vyote vilivyosalia vya Mkoa huo.
Dkt.
Kalemani alizindua Mradi huo Juni 19, 2021 katika kijiji cha
Namtumbuka, Mtwara Vijijini akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara Dunstan Kyobya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, Wabunge, Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius
Kalolo, Mjumbe wa Bodi hiyo Oswald Urasa, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa Wakala, Mhandisi Jones Olotu pamoja na viongozi na wataalam
mbalimbali wa Wizara, REA na TANESCO.
Akizungumza na wananchi
wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi, Waziri Kalemani alieleza kuwa lengo la
Mradi husika ni kupeleka umeme katika vijiji 384 vya Mkoa wa Mtwara
ambavyo havijafikiwa na nishati hiyo.
“Mkoa wa Mtwara una vijiji
vyenye umeme 413 kati ya 797. Kwa kutambua hilo, leo ninawakabidhi
wakandarasi waushambulie mkoa huu kwa pamoja na kuhakikisha vijiji vyote
vilivyosalia vinapatiwa umeme katika mradi huu,” alisema Waziri.
Alisema
Mradi umefadhiliwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia hivyo
akaishukuru Taasisi hiyo na kwa niaba ya Serikali akaahidi kuimarisha
uhusiano mzuri baina ya pande hizo mbili.
Waziri Kalemani
aliwataka wananchi wa Mtwara kuutumia umeme huo katika shughuli za
kimaendeleo ili kuboresha maisha yao na hali ya kiuchumi ya nchi kwa
ujumla.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi, Wakili Kalolo
alieleza kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeandaa Mpango Kazi wa
Miaka Mitano uliojikita katika kufanikisha malengo ya Serikali ya
kusambaza nishati ya umeme katika vijiji vyote ifikapo Disemba 2022 na
vitongoji vyote mwaka 2025.
Alisema kuwa Mpango Kazi huo ni wa
miaka mitano kuanzia 2021/22 hadi 2025/26 na umejikita katika kufikisha
umeme kwa Watanzania wote, maeneo ya viwanda, madini, kilimo, uvuvi na
ufugaji.
“Mheshimiwa Waziri, Mradi huu unaouzindua leo ni sehemu
tu ya Mpango Mkakati wa Wakala na umelenga kusambaza umeme katika vijiji
1956 ambavyo havijafikiwa na miundombinu ya umeme,” alibainisha.
Alieleza
zaidi kuwa Mradi utatekelezwa katika mikoa 24 ambayo imegawanywa katika
mafungu 39 na kwamba unakadiriwa kugharimu takribani shilingi trilioni
1.3 ambapo unatarajiwa kukamilika Disemba, 2022.
Wakili Kalolo
aliongeza kuwa Mradi utakapokamilika utawezesha vijiji vyote 12,268
kupatiwa umeme na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kwa Ukanda wa
Kusini mwa Jangwa la Sahara kufikisha umeme katika vijiji vyote.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu,
aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Wakala, alieleza kuwa katika Mradi
huo mkoani Mtwara, wateja wa awali 6,182 wataunganishwa.
Aliongeza
kuwa utekelezaji wa Mradi katika Mkoa huo utagharimu shilingi bilioni
62.146 ambapo utatekelezwa na Mkandarasi Namis Corporate Engineers and
Contractors katika Wilaya ya Masasi na Nanyumbu na Mkandarasi Central
Electricals Internationals katika Wilaya ya Mtwara Vijijini, Newala na
Tandahimba.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya, alisema
umeme una umuhimu wa pekee katika Mkoa wa Mtwara kwani pamoja na kuwa ni
fursa katika shughuli za kimaendeleo lakini pia ni muhimu kwa shughuli
za kiusalama ikizingatiwa kuwa mkoa huo uko pembezoni mwa nchi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, baadhi ya Wabunge wa Mtwara, Geofrey Mwambe
(Ndanda), Issa Mchungahela (Lulindi), Katani Katani (Tandahimba), Hassan
Mtenga (Mtwara Mjini) na Abdallah Chikota (Nanyamba) walipongeza
jitihada zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu
katika kuwapelekea wananchi wake maendeleo kupitia usambazaji umeme
vijijini.
Aidha, wawakilishi hao wa wananchi waliipongeza Wizara
ya Nishati, REA na TANESCO kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya
kuhakikisha Mtwara inafikiwa na umeme katika pande zote.
Waliwataka
wakandarasi waliopewa dhamana ya kutekeleza Mradi husika kuhakikisha
wanafanya kazi hiyo kwa uaminifu na weledi huku wakiwahakikishia kuwa
watawasimamia ipasavyo ili wasiiangushe Serikali na wananchi.
Monday, June 21, 2021
WAZIRI KALEMANI AZINDUA REA III AWAMU YA PILI MTWARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment