Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw.Tumaini Nyamhokya akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (Talgwu) Bw. Rashid Mtima akizungumza Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania (Talgwu) wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV,
WATUMISHI wa kutoka kada mbali mbali wanaogombea nafasi mbali za uongozi wa chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TAWLGU) wameaswa kuridhikaxs na matokeo badala ya kushindwa na kwenda kuanzisha chama chao kipya.
RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini,(TUCTA),Tumaini Nyamhokya ameyasema hayo leo Juni 22, 2021 wakati akifungua mkutano Mkuu wa TAWLGU mkoa wa Dar es Salaam ambao unaendana na uchaguzi wa viongozi wa mkoa huo, Nyamhokya alisema ni vema viongozi kukaa meza moja huku wakiimba wimbo mmoja ambao watakubaliana kwa hoja bila kwenda kwenye migomo au kuingia barabarani
Amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi wa viongozi wanaposhindwa katika chaguzi kuwa na makovu ya kushindwa uchaguzi hivyo kuunda makundi ndani ya Chama jambo ambalo hudhoofisha chama
Amesema kukaa kwa pamoja baina ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa ngazi ya mkoa na Taifa kwa pamoja na kuwa wamoja ni chachu mmojawapo kuwa wanauwezo wa kutatua changamoto zinazowakabili wanachama wake.
"Ni vema viongozi wakakaa meza moja huku wakiimba wimbo mmoja ambao watakubaliana kwa hoja bila kwenda kwenye migomo au kuingia barabarani." Amesema Nyamhokya.
"Hatuzuiwi kuingia kwenye migomo au kuingia barabarani lakini kukaa mezani, kujadiliana na kupata ufumbuzi wa mambo yetu ni mafanikio makubwa na kutafanya uwepo wa kusikilizana baina ya viongozi wa Taifa na Chama na kufanya vyama kuwa imara zaidi." Amesema
Ameongeza kuwa, ni matarajio yake makubwa kuwa katika uchaguzi wa leo watapatikana viongozi wazuri ambao watakiongoza Chama kwa kusikilizana na kukunaliana katika hoja mbali mbali watakazokuwa wanaafikiana.
Naye, Rashid Mtima Katibu Mkuu wa TAWLGU amesema mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano ni mkutano wa kikatiba ambao lengo lake ni kupitia taarifa za Chama za kazi na kifedha kwa miaka mitano iliyopita.
"Leo tutakaa na kupitia ripoti ya miaka mitano katika Mikoa wa Dar es Salaam pia tutachagua viongozi wapya wa a miaka mingine mitano akiwamo Mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam."Amesema Mtima.
" Katiba imeipa Mamlaka Chama kuanzisha mkoa tangu mwaka jana ambapo baraza kuu liliidhinisha Mikoa mitatu ya Dar es Salaam iianzishwe ikiwemo mkoa wa Temeke,ilala na Kinondoni hivyo leo wanafanya uchaguzi wa mkoa wa Dar es Salaam lakini wakitoka hapa wataenda kuchagua viongozi wa Mikoa mitatu ilihuduma kwa wanaachama ifike vizuri katika kuwahudumia."Alisema
"Kanuni za chama za mwaka 2018 zinazungumza kwamba viongozi wakichaguliwa wanapaswa kupewa mafunzo ya uongozi ya shughuli za Chama hivyo viongozi watakaochagulia leo hapa watapewa mafunzo ya Uongozi kwa shuguli zote Chama cha wafanyakazi." Amesem
No comments:
Post a Comment