KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imekabidhi zawadi kwa washindi waliopatikana kupitia kampeni ya Twende Mjini na M-Pesa, kampeni inayoendeshwa kwa malengo ya kurudisha kwa jamii pamoja na kuhamasisha jamii kutumia huduma za mtandao huo ambazo zinaboreshwa kila siku.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Afisa Tarafa kutoka Manispaa ya Kinondoni Bi. Rahma Kondo amesema Vodacom imekuwa sehemu ya jamii kwa kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii pamoja na kutoa huduma za mawasiliano katika maeneo mengi ya miji na vijiji.
Aidha amewataka watanzania kujiunga na mtandao wa Vodacom katika Mawasiliano na kujipatia nafasi ya kujishindia zawadi maalumu ambazo wamekuwa wakizitoa kwa wateja wanaotumia huduma mbalimbali zinazotolewa na mtandao huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya Dar es Salaam Brigitha Steven amesema si vigumu kushinda wateja na mawakala wanaweza kushinda kwa kutumia huduma za M-Pesa kupitia *150*00# au kupitia M-Pesa App kwa kufanya miamala ya kutuma pesa, kulipa bili na huduma mbalimbali na moja kwa moja wataingia kwenye droo na kuweza kuwa washindi.
Pia amewataka wateja wa mtandao huo kupokea namba ya huduma kwa wateja 0754 100 100 ili kutopitwa na bahati zao na wataendeleza kampeni ya kujitambulisha kwa wateja kupitia jumbe fupi 'Sms' pamoja na mitandao ya jamii ili wateja na watumiaji wa huduma za M-Pesa wasipitwe na zawadi hizo.
Kampeni ya Twende Mjini na M-Pesa itaendeshwa kwa wiki nane ambapo kila siku mshindi wa bodaboda mpya aina ya Boxer BM 125X atapatikana na mshindi mmoja wa bajaji mpya aina ya TVS King GS atapatikana kila wiki huku katika Grand Finale ya mashindano hayo mshindi atajishindia gari jipya aina ya Toyota Corolla Cross (SUV) ya mwaka 2021.
Katika droo hiyo ya kwanza kati ya droo nane waliojishindia bodaboda ni Godfrey Mgeni (Morogoro,) Francis Kwale, Wakala wa huduma za M-Pesa (Dar es Salaam,) Zanzibar gateway Wakala wa huduma za M-Pesa (Zanzibar,) Ramadhan Nkondo (Dar es Salaam) Pili Joseph (Dar es Salaam.) huku Bajaji mpya ikienda kwa Nyangije Basondole kutoka Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment