HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 4, 2021

Takwimu za Wami Ruvu Zinaisaidia Serikali Kuchukua Tahadhari za Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi-Jafo

 WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo, amesema takwimu zinazotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu ni Muhimu kwa Sababu zimekuwa zikiisaidia Serikali hususani Wizara yake kuchukua Tahadhari kuhusu suala zima la Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye vyanzo vya maji ikiwemo Mito na Mabwawa.


Waziri Jafo ametoa kauli hiyo Mjini Dodoma kwenye Wiki ya mazingira alipotembelea Banda la Maoensho la Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu.

Amesema Rasilimali maji ni Muhimu kwa maendeleo na Ustawi wa Binadamu, hivyo ameitaka Bodi hiyo ya Maji katika Bonde la Wami Ruvu kuwa mstari wa Mbele kuiongoza Serikali kupitia Takwimu zake ili iweze kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na athari za Mazingira kwenye vyanzo vya Maji.

“ Ofisi yenu ni muhimu sana, lakini inatusaidia vile vile kutoa tahadhari watu wasivamie vyanzo vya maji Kwa Sababu wakivamia Mambo yote yanakuja kuharibika, kwa mfano leo hii tunajenga lile bwana la Nyerere kama watu watavamia vyanzo vya Maji lile bwana litakuwa halijai.” Alisisitiza Wazir Jafo.

Kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani kinatarajia kufikia kilele chake June 5, ambapo Serikali inatarajia kuzindua Kampeni Kabambe ya Kuhamasisha Jamii Kutunza na Kulinda Mazingira.

Waziri wan chi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Jamii wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, kuhusiana na Shughuli mbalimbali za Bonde hilo ikiwemo Utunzaji wa Mazingira na Ulinzi wa vyanzo vya Maji, Utoaji Vibali wa Matumizi ya Maji ya Visima, Mito na Mabwawa, pamoja na Utoaji Elimu kwa Jamii ili kuepusha Migogoro ya Maji.
Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akisaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Wageni Katika Banda la Maonesho la Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, alipotembelea Kwenye Banda hilo ili kujionea Shughuli mbalimbali za Bodi hiyo, Pemebeni yake ni Afisa Kutoka Bodi hiyo Harold Kayoza.
Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, alipofika kwenye Banda la Maonesho la Bodi hiyo ili kujionea Shughuli mbalimbali za Bodi hiyo kwenye Suala zima Utunzani wa mazingira kwenye vyanzo vya Maji, Utoaji Vibali wa Matumizi ya Maji ya Visima, Mito na Mabwawa, pamoja na Utoaji Elimu kwa Jamii ili kuepusha Migogoro ya Maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad