Na Mwandishi Wetu, Lushoto
UMOJA
wa Maendeleo wa Usambara (UDI), umesema utamuunga mkono Mkuu mpya wa
Wilaya ya Lushoto, Kalisti Lazaro ili kuharakisha maendelea ya wilaya
hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa umoja huo wa
Usambara Development Initiative (UDI) mwenyekiti wa umoja huo Ali Daffa
alisema wamefurahishwa na hatua nzuri ya mashirikiano baina ya umoja huo
na serikali.
Daffa alimshukuru kwa kukubali wito wao wa kuja
kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa UDI na kumhaidi kumpa ushirikiano
katika shughuli za kuwalete Wananchi wa Lushoto Maendeleo.
"Kiukweli
mkuu wa wilaya tumefurahishwa na mashirikiano uliyoyaonesha kwetu
tumekualika muda mfupi sana umekuja lakini umeaahidi tutakuwa pamoja
katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Lushoto na sisi tunakuaahidi
tutakuwa na wewe bega kwa bega kuhakikisha tunafanya kazi pamoja, "
alisema Daffa.
Umoja huo wenye zaidi ya wanachama 150 waliopo
ndani na nje ya nchi, umekuwa ukisaidia kutatua changamoto mbalimbali
wilaya hiyo katika huduma za jamii.
Umoja huo ambao unajumuisha
Wadau wa Maendeleo kutoka maeneo ya Usambara (Lushoto, Mlao, Bumbuli)
wanaoishi maeneo mbalimbali ya Nchi na Nje ya Nchi, umekuwa mahususi
kushughulikia changamoto za wananchi ikiwemo kukarabati shule za wilaya
hiyo.
Umoja huu umekuwa ukisaidia Jamii ya watu wa Lushoto
katika Njanja mbalimbali za Maendeleo kama kuboresha huduma za jamii,
ukarabati wa shule, uboreshaji wa huduma za afya.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya amewapongeza viongozi na wanachama
wa UDI na kuhaidi kuwapa ushirikiano wa dhati katika kuwaletea Wananchi
wa Lushoto Maendeleo.
Pia aliwaasa wana UDI kudumishi umoja, mshikamano, upendo na kutobaguana kwa itikadi za kisiasa, dini na ukabila.
Pia
Wana UDI walimzawadia Mkuu wa Wilaya zawadi ya Kofia na Tshirt ambazo
zimekuwa na nembo ya UDI pamoja na kumpa kitabu cha Dhahabu ya Amani.
Wana-UDI wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya Kalisti Lazaro mara baada ya kufungua mkutano wao mkuu wa mwaka
Mkuu wa wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro (aliyevaa kofia) akifurahia jambo pamoja na viongozi wa UDI. Kulia kwa mkuu wa wilaya ni Katibu wa CCM wilaya Ramadhani Mahanyu, ofisa wa UDI na kulia ni Ali Daffa
Mwenyekiti wa UDI Ali Daffa akimkabidhi kofia na t-shirt mkuu wa wilaya kama ishara ya kumkaribisha katika wilaya hiyo
No comments:
Post a Comment