Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezindua awamu ya pili ya utengenezaji wa magari aina ya HONG YANG katika kiwanda cha GF Assemblers Kibaha mkoni Pwani
Akizungumza baada ya uzinduzi wa magari hayo, Kunenge alikemea baadhi ya tabia za watendaji wa serikali za kupishana katika ofisi za wawekezaji kwa visingizio mbali mbali mbali
Ikiwamo kulazimisha kuonana na wamiliki ama kwa visingizio vya kutaka kufanya ukaguzi hali inayowafanya wawekezaji kuwa na hofu na kujikuta wanashindwa kutimiza majukumu yao
Kunenge alisema Serikali ya mkoa wa Pwani inahakikisha inapata maendeleo kwa kuongeza fursa ya biashara na uwekezaji wenye mazingira rafiki na utawala bora kwa hiyo hataki kusikia ama kuona watendaji wanakua kikwazo katika kufanikisha mpango huo na kwamba hatawavumilia.
" wakati Serikali ikijenga mazingira rafiki na wawekezaji sisi wenyewe mafisa wa Serikali tumekuwa kikwazo , Nae Meneja wa kampuni GF Vehcle Assemblers , Ezra Mereng alisema lengo lao ni kuunda kila aina ya chapa (brand ) ya magari kwa kuwa teknolojia na mitambo waliyonayo inauwezo wa kuunganisha magari aina zote zenye viwango na vigezo vya kitaifa na kimataifa.
Mereng alisema kiwanda hicho kilianza kwa kuunda magari chapa aina ya FAW na sasa wamezindua chapa ingine ya Hongyan na kuwataka wadau na makampuni mengine ya magari kuacha kuagiza badala yake walete GFA kuundiwa (Assembling) kwa zingatia vigezo vyoote vya kimataifa.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akipokea zawadi ya kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya GF Assemblers Imrani Karmali wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari jipya ya kubebea mizigo anina ya Hong Yang katika kiwanda hicho leo mkoani Pwani.Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifurahia jambo na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha GF Assemblers,Imrani Karmali baada ya uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari mpya ya kubebea mizigo aina ya Hong Yan katika kiwanda hicho mkoani Pwani
No comments:
Post a Comment