HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 16, 2021

RC IBUGE akagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji kupitia ziwa Nyasa

 


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amefanya ziara ya pili ya kukagua maeneo ya mipakani kwa kutembelea mpaka wa Chiwindi mwambao mwa ziwa Nyasa unaogawa Tanzania na nchi ya Msumbiji.

RC Ibuge katika ziara hiyo aliongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyasa.

Akizungumza na viongozi na watendaji wa serikali katika kijiji cha Chiwindi,wilayani Nyasa,RC Ibuge ameagiza ulinzi na usalama katika eneo la mpaka kuimarishwa zaidi ili wananchi wanaoishi mpakani wasiwe na hofu bali waendelee kushiriki katika kazi za uzalishaji mali.

Amewatahadharisha viongozi na watendaji waliopo mpakani wasiruhusu vitendo ambavyo vinahatarisha amani katika mipaka ya nchi ukiwemo mpaka wa Chiwindi ambako kuna mwingiliano wa wageni kutoka Msumbiji na kuingia Tanzania.

Ameitaja Mipango ya serikali ni mikubwa, na kueleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan ana lengo la kuiendeleza Tanzania ili ipige hatua kubwa katika maendeleo.

Hata hivyo amesema bila amani na utulivu hakuna maendeleo.

Hii ni ziara ya pili ya RC Ibuge kukagua maeneo ya mipaka katika Mkoa wa Ruvuma,ambapo katika ziara ya kwanza RC Ibuge alikagua mpaka wa Mkenda unaoigawa Tanzania na Msumbiji kupitia Mto Ruvuma wilaya ya Songea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad