HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 18, 2021

NMB YAKABIDHI SERIKALI HUNDI YA ZAIDI YA BILIONI 21.7

 

Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango (wapili toka kulia) akionesha mfano wa hundi ya zaidi ya sh Bilioni 21.8 iliyokabidhiwa Serikali ikiwa ni gawio kutoka Benki ya NMB,kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori .

*************************

Benki ya NMB imetoa gawio la Sh21.8 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 ya gawio la mwaka jana ambalo lilikuwa Sh15.25 bilioni.


Akipokea mfano wa hundi, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema kiasi hicho kimemridhisha kwa mwaka huu lakini akataka waongeze maarifa zaidi ili kutoa gawio la juu ikiwemo kuwekeza katika nchi majirani.

Dk Mpango alisema kiwango kilichotolewa mwaka jana hakikumfurahisha ndiyo maana akaagiza lazima waongeze juhudi lakini kwa mwaka huu amebarikiwa.Gawio lililotolewa jana ni sehemu ya faida ya Sh206 bilioni ambazo benki hiyo ilipata katika msimu wa kuishia desemba 2020 baada ya kuondoka kodi.

Serikali inapokea gawio hilo kutokana na umiliki wake wa hisa asilimia 31.8 ndani ya benki hiyo ambayo kwa miaka 8 mfululizo imekuwa ikipata tuzo ya benki bora nchini.

“Nimefurahishwa sana na hiki mlichotoa, pamoja na mafanikio haya lakini nataka muongeze ubunifu ili mwaka muwe zaidi ya hapa, hata hivyo nakuagiza Waziri wa Fedha kwamba kiasi hiki kikafanye kazi nzuri kwa wananchi ambayo imekusudiwa,” amesema Dk Mpango.

Kuhusu NMB aliwataka kushirikiana na Taasisi zingine ili wakae na benki Kuu (BoT) kujadili kuhusu riba kubwa ambayo bado inatozwa na mabenki na hivyo kusababisha watu washindwe kukopa.

Aliwataka viongozi wa taasisi ambazo Serikali ina hisa lakini hawatoi gawio kwamba wajitathimini vinginevyo watachunguzwa na watakaokuwa wamekiuka kanuni Serikali itawapeleka Segerea hata kama kumejaa.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NMB Edwin Mhede alisema tayari fedha hizo zilishawekwa katika akaunti ya msajili wa Hazina na kwamba mwakani watakuwa na kiasi kikubwa zaidi kutokana na mwenendo wavyoona.

Mhede alitaja siri kubwa ya mafanikio ya NMB ni ubunifu na kutljituma kwa watumishi wao katika kuutafuta masoko lakini utoaji bora wa huduma unaowabutia watu kuitumia benki hiyo.

Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna alisema mbali na gawio hilo,lakini wamelipa Serikalini Sh245 bilioni kama kodi za tozo mbalimbali na kutumia asilimia moja ambayo ni zaidi ya Sh2 bilioni kwenye huduma za kijamii.

Bi. Zaipuna alisema benki hiyo imefikia mtaji was Sh1.1 trilioni kutoka Sh660 bilioni kwa mwaka 2015 hivyo ukuaji wake unatia matumaini kwamba itaendelea kuwa ni benki bora yenye kutoa huduma kwa viwango vinavyotakiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad