Na Amiri Kilagalila,Njombe
BWENI la wasichana shule ya Sekondari Ikuwo wilayani Makete mkoani Njombe limeteketea kwa Moto huku ikisadikika chanzo chake kuwa ni hitilafu ya Umeme au mkaa ulioanzia Chumba cha Matron (Mlezi wa wanafunzi)
Moto huo ulioanza asubuhi leo majira ya saa moja umeteketeza vitanda vitanda, magodoro, nguo za wanafunzi pamoja na vifaa vyao huku wanafunzi wote wakiwa salama
Jumla ya thamani ya vitu vilivyoteketea bado haijajulikana huku tathmini ikiendelea kufanyika.
Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, Mkurugenzi mtendaji wilaya na wataalamu mbalimbali wamefika kuangalia mali zilizoteketea kwa Moto huo uliotokea
Chanzo:Kitulo FM
No comments:
Post a Comment