Viongozi wa Kampuni ya HEBO na Shirika la Usimamizi wa Miradi (Project Management Institute (PMI), tawi la Tanzania wakisaini mkataba wa makubaliano kati ya taasisi hizo mbili, tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Slipway Terrace.
Rais wa Shirika la Usimamizi wa Miradi (Project Management Institute (PMI), Tanzania, Ella Naiman akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar es Salaam leo huku wakitia saini mkataba wa makubaliano wa kati ya taasisi hizo mbili, tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Slipway Terrace.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa progamu za mafunzo HEBO Consult, Bulla Hekeno akizungumza na waandishi wa haari Mkoa wa Dar es Salaa leo wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano kati ya taasisi hizo mbili, tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Slipway Terrace.
Rais Mstaafu wa PMI Tanzania, Anael Ndosa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Bodi ya PMI Tanzania, Daniel Materu akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja.
Picha ya pamoja.
*Waungana ili Kukuza uchumi wa nchi.
KAMPUNI ya HEBO kupitia kitengo chake cha mafunzo na ushauri wa kibiashara (HEBO Consult) imeingia makubaliano na Shirika la Usimamizi wa Miradi (Project Management Institute (PMI), tawi la Tanzania kutoa mafunzo kwa waratibu na wasimamizi wa miradi yatakayokidhi viwango vinavyotambulika Kimataifa.
Akizungumza leo Juni 2, 2021 na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano kati ya taasisi hizo mbili, tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Slipway Terrace, Rais wa PMI Tanzania, Ella Naiman amesema kuwa mafunzo hayo ya usimamizi wa miradi yatasaidia kuleta chachu na hamasa katika fani ya uendelezaji wa miradi kwa kupitia mafunzo na mitaala iliyotayarishwa na kutambuliwa na Shirika la Usimamizi wa Miradi (Project Management Institute-(PMI) na shirika linalosimamia mafunzo na kutoa vyeti vya ukufuzi katika usimamizi wa miradi duniani kote.
“Kama inavyofahamika, Tanzania tupo katika harakati za kujenga uchumi wa viwanda unaopelekea uwekezaji mkubwa katika miradi ya maendeleo na hii inamaanisha kuna uhitaji mkubwa wa kuwa na wasimamizi wa miradi wenye vigezo vya juu vinavyotambulika kimataifa, ili kuhakikisha ufanisi katika kutekeleza na kukamilisha miradi hii ya kuleta maendeleo katika taifa letu inafanikiwa.”
Licha ya hayo Ella amesema kuwa Makubaliano hayo kati ya PMI Tanzania na HEBO Consult, yanategemea kuongeza uwezo wa wasimamizi wa miradi na waendesha miradi katika ngazi na sekta tofauti.
“Cheti hiki humuweka mtaalam wa usimamizi wa miradi katika jukwaa la dunia na kumpa vigezo vinavyotamvulika na wawekezaji wa kimataifa wanaoanzisha na kuendesha miradi ya maendeleo katika sekta zote nchini. Wataalamu wanaofuzu mafunzo haya na kupata vyeti vya PMP wanakuwa na uwezo wa kusimamia miradi ya aina tofauti katika viwango vya kimataifa vinavyotambulika.” Amefafanua Bulla
Amesema kuwa Wanachama wa PMI Tanzania watanufaika na makubaliano haya kwa namna ya Punguzo katika mafunzo kutoka HEBO Consult hadi asilimia 20% pamoja na usaidizi wa karibu kujiandaa na mitihani ya vyeti vya ufanisi.
Amesema kuwa HEBO Consult ni kampuni ya kwanza Tanzania kupata Kibali cha Premier ATP (Authorized Training Partner) wa PMI kiachowawezesha kutoa mafunzo ya Usimamizi wa Mradi yaliyotayarishwa na kuratibiwa na PMI Africa nzima.
No comments:
Post a Comment