Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Godfrey Mwambe akizungumza na wafanyabiashara wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuhusiana na fursa zilizopo za Uwekezaji nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi-Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza fursa zilizopo katika sekta ya Mifugo kwa Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt.Godwill Wanga akizungumza kuhusiana na mikakati ya baraza hilo katika ukuzaji wa biashara nchini.
Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Manfredo Fanti akizungumza kuhusiana na na majadilioano kati ya Serikali ya Tanzania na Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya uliofanyika jijini Dar es Salaam.
*Awahakikishia fursa za Uwekezaji nchini na milango iko wazi .
*EUBG wafurahishwa kukutana na viongozi wa Serikali ya Tanzania kufanya majadiliano.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Uwekezaji, Godfrey Mwambe amesema kuwa Tanzania ina fursa za Uwekezaji na kutaka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuja kuwekeza na milango iko wazi.
Mwambe aliyasema hayo wakati alipokutana katika kikao cha majadiliano na Wafanyabiashara wa Jumuiya Umoja wa Ulaya kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwambe alisema kuwa Serikali ya Tanzania kuwezesha taratibu kwa wafanyabiashara kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Nae Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi-Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel amesema sehemu ya Uwekezaji ni Sekta ya mifugo kwani Tanzania kwa upande wa Ngozi na nyama ambapo Masoko wanaweza kufanyia katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.
Profesa Ole Gabriel amesema kuwa nchi za jumuiya za Ulaya wana akiba fedha ambao wanaweza kuwekeza na nchi ikaweza kupata fedha za kigeni pamoja kuongeza ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EUBG), Cikay Richards alisema ujio wa Umoja huo ni kufanya majadiliano na Serikali ya Tanzania katika kuangalia namna ya fursa ya za Uwekezaji zilizopo Tanzania.
Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Manfred Fant amesema kuwa majadiliano na Serikali ya Tanzania yanafungua milango kwa wafanyabiashara kuwekeza Tanzania.
Amesema kuwa katika Uwekezaji huo wataongeza Maendeleo ya nchi katika ukuaji wa uchumi kupata fedha za kigeni.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga amesema kuwa TNBC ni kutaka kuongeza biashara nyingi ambapo EUBG wakiwekeza wanakuwa wameongeza ajira pamoja na kuongeza fedha za kigeni.
Dkt.Wanga amesema kuwa kumekuwa na hatua mbalimbali za serikali katika kutatua changamoto ziliopo katika sekta binafsi.
No comments:
Post a Comment