HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 24, 2021

SALHA KUSINDIKIZA USIKU WA PAMBE ZA VIJORA BURUNDI

 

**********************

Na.Khadija Seif Michuzi Tv  

MSANII wa Taarab Salha Abdallah Kuwasha Moto Burundi. Akizungumza na Michuzi Tv Nadia Khamis ambae ni Mdau Mkubwa wa Muziki wa Taarab amesema Show hiyo inalenga kunyanyua Muziki huo pamoja na kuusukuma hata nchi zingine zifahamu kuwa Tanzania Kuna Muziki wa aina hiyo.

"Kupitia Mimi ningetamani kuona Muziki wa Taarab unafika mbali zaidi kujulikana na kujitangaza ili tuweze kupata nafasi ya kuonyesha upekee tulionao na Sauti za kipekee kutokana nchini kwetu."

Aidha,Nadia ameeleza kuwa katika show hiyo aliyoipa jina la "Pambe za vijora"  Sababu ya Kumchagua Salha Abdallah kama Mtumbuizaji sanjari na Bendi ya Taarab ya  Jasmini.

"Ni Msanii ambae Nina ukaribu nae napenda kazi zake hivyo ni wapenzi wa Bujumbura nchini burundi kusubiri Julai 27 mwaka huu kuona Salha akitumbuiza Mubashara jukwaani.

Pia amesema show hiyo ni moja ya zawadi kwa nchi ya Burundi kutokana na takribani miaka 14 kutokuwepo kwake huko kwani ni  sehemu ya Makazi yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad