Katibu Tawala wa Mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam na mwenyekiti wa kamati ya Maafa ya kimkoa, Paulo Mshimo Makanza amefunga mradi wa Jipange(Jipange Project) uliokuwa na lengo la kutoa mafunzo kwa
kwa kata 12 zilizopo katika Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Ilala.
Akizungumza kwenye mkutano huo Katibu tawala Makanza ameushukuru uongozi wa mradi wa Jipange(Jipange Project) kwa kutoa elimu ya namna ya kujiandaa kwenye kujikinga na maafa kabla ya kutokea ambayo imenufaisha kata zipatazo 12 za Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Ilala.
Mgeni
rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam na mwenyekiti wa
kamati ya Maafa ya kimkoa, Paulo Mshimo Makanza akizungumza na wajumbe
wa kamati za maafa wa Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Ilala wakati wa
kufunga programu ya mafunzi kwa kata 12 kuhusu namna ya kujiandaa na
maafa na namna ya kukabiliana na maafa hayo katika jamii.
Meneja
wa Mradi wa Jipange Shamim Zakaria akiwasilisha mada kwa wajumbe wa
kamati za maafa wa Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Ilala kuhusu namna
walivyoweza kufanikisha utoaji wa elimu kwenye kata 12kuhusu namna ya
kujikinga na maafa kabla ya kutokea na baada ya kutokea kupitia mradi wa
Jipange(Jipange Project) pamoja na kutoa mipango mikakati ya uratibu wa
Maafa kwa wajumbe hao.
Ofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Idara ya Uratibu wa Maafa, Charles
Msangi akitoa mada kuhusu sheria za usimamizi wa maafa katika ngazi za
kijiji mpaka kitaifa wakati wa ufungaji wa mradi wa Jipange kwa kwa
wajumbe wa kamati za maafa wa Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Ilala.
Mgeni
rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam na mwenyekiti wa
kamati ya Maafa ya kimkoa, Paulo Mshimo Makanza(wa tatu kushoto)
akiwakabidhi mipango mikakati ya uratibu wa maafa kwa baadhi ya wajumbe
wa kata wa kamati za maafa wa Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Ilala
wakati wa kufunga mradi wa Jipange
Mgeni
rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam na mwenyekiti wa
kamati ya Maafa ya kimkoa, Paulo Mshimo Makanza(wa tatu kushoto)
akiwakabidhi vifaa vya huduma ya kwanza baadhi ya wajumbe wa kata wa
kamati za maafa wa Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Ilala wakati wa
kufunga mradi wa Jipange
Baadhi
ya wajumbe wa kamati za maafa wa Manispaa ya Kinondoni na Jiji la
Ilala wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa kufunga mradi wa
Jipange.
Mratibu
wa Maafa wa manispaa ya Kinondoni, Pendo Fredy akitoa shukrani kwa
mgeni rasmi pamoja na viongozi wa mradi wa Jipange uliowezesha mafunzo
ya kwa kata 12 kuhusu namna ya kujikinga na maafa kabla ya kutokea na
baada ya kutokea kwa wajumbe wa kamati za maafa wa Manispaa ya
Kinondoni na Jiji la Ilala.
Mgeni
rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam na mwenyekiti wa
kamati ya Maafa ya kimkoa, Paulo Mshimo Makanza(wa tatu kushoto) akiwa
kwenye picha za pamoja na Baadhi ya wajumbe wa kamati za maafa wa
Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Ilala pamoja na viongozi wa mradi wa
Jipange( Jipange Project)
No comments:
Post a Comment