

MKURUGENZI
Mkuu wa TASAF.Ndg.Ladislaus Mwamanga akitowa maelezo ya mafanikio ya
Mradi wa Tasaf, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati walipofika
Ikulu Jijini Zanzibar Ujumbe wao ukiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Mohamed Omary
Mchengerwa, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu
Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MKURUGENZI
wa Mkuu wa Mkurubata Dkt.Seraphia Mgembe akizungumza wakati wa mkutano
wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) walipofika Ikulu Jijini
Zanzibar kwa mazungumzo wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Omary
Mchegerwa na Maofisa wengi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa
Ikulu.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ukiongozwa na Waziri wa wizara hiyo (MB) Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment