Benki ya CRDB na Mfuko wa Bima ya Taifa NHIF imeendelea na utekelezaji 
wa tumeanza utekelezaji wa mpango wa “Ushirika Afya” kwa  kuingia 
makubaliano na Chama Kikuu cha Ushirika cha maziwa mkoani Tanga kwa 
ajili ya kuwapatia bima ya afya wanachama wake mkoani humo ambao ni 
wazalishaji wa maziwa kama sehemu ya mpango wa Ushirika Afya.
Mgeni Rasmi wakati wa Kuingia Makubaliano hayo Mkuu wa Wilaya ya Tanga 
Mh. Thobias Mwilapwa amewapongeza benki ya CRDB na Mfuko wa Bima ya afya
 ya Taifa kwa Ubunifu wa mpango huo ambao utawafaidisha wakulima wengi 
nchini “ Nasihi wanaushirika katika mkoa wa Tanga Kutumia Fursa hii 
tujiunge kwa wingi kwenye vyama vya ushirika ili kutumia fursa hii 
kuboresha maisha ya familia zetu” Mh. Mwilapwa
Kwa niaba ya Benki ya CRDB Afisa Biashara Mkuu  Dkt. Joseph Witts 
alisema Katika Makubaliano hayo Benki ya CRDB itawawezesha wanachama wa 
chama kikuu kulipia bima ya Afya bila riba yoyote na hivyo kuboresha 
uzalishaji wa maziwa katika mkoa wa Tanga.” Huu ni mpango maalumu wa 
Benki yetu unaolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika 
maisha ya wateja wetu walioko kwenye sekta ya Kilimo nchini kote” 
alieleza Dkt. Witts.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa NHIF Bw. Christopher Mapunda alisema 
kuwa mfuko wa Bima ya taifa katika mkakati huu unalenga kuboresha 
upatikanaji wa huduma za Afya kwa wakulima na wafugaji nchini. “Mpango 
utawawezesha wazalishaji wa maziwa kupata huduma za afya katika vituo 
zaidi ya Elfu nane katika nchi nzima” alieleza Bw. Mapunda
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa maziwa mkoani Tanga Nd. Shamte
 Said amewashukuru Benki ya CRDB na NHIF kwa kuja na mpango huo “ 
Nawapongeza kwa kuwakumbuka wazalishaji wa maziwa nawahidi tutatumia 
fursa hii kujihakikishia upatikanaji wa matibabu” Ndg. Shamte
Hafla ya utiaji sahihi wa makubaliano hayo ulihudhuriwa na Mrajisi 
Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga, Maafisa wa Mfuko wa Bima 
ya Taifa, Maafisa wa Benki ya CRDB na Wajumbe Wa Bodi ya Chama Kikuu cha
 Ushirika wa Maziwa Tanga.
Utekelezaji wa mpango wa Ushirika Afya ulianza mapema wiki iliyopita 
ambapo Benki ya CRDB na NHIF waliingia mkataba wa makubaliano na na 
vyama vya ushirika vya CHUTCU kilichopo wilaya ya Chunya, vyama vya MCU 
na MWAMARU vilivyopo wilaya ya Rungwe, Mbeya.
Katika mpango huu Benki ya CRDB inasidia kurahisisha upatikanaji wa bima
 za afya kwa wakulima waliopo katika vyama vya ushirika (AMCOS) kupitia 
huduma ya mkopo wa gharama za bima iliyopewa jina "Ushirika Afya Premium
 Loan." Huduma hiyo inatolewa bila makato wala riba. Mkulima anaruhusiwa
 kukata bima yake, pamoja na wategemezi wake ikiwamo mke/ mume na 
watoto.
 

 
 




 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment