Na.Catherine Sungura, WAMJW-Kilimanjaro
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy
Gwajima, leo ametembelea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) ikiwa ni kufuatilia utekelezaji wa muongozo namba 7 wa ushauri wa
wasafiri wanaoingia nchini uliotolewa tarehe 4 Mei, 2021.
Katika
muongozo huo moja ya maelekezo ni kufanya uchunguzi wa COVID-19 kwa
kuwapima kipimo cha haraka (Rapid Test) wasafiri wote wanaoingia nchini,
kwani kumekuwa na malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi kuhusu zoezi
hilo. Mojawapo ya malalamiko hayo ni abiria kuchelewa kumaliza hatua za
huduma ya vipimo vya afya.
Mhe. Waziri amebaini kuwa watumishi
wapo na wanafanya kazi zao vizuri wakiwemo maafisa afya, maabara na
watumishi wa uwanja wa ndege. Waziri amewapongeza watumishi hao kwa kazi
nzuri wanaoifanya. Aidha, amewashukuru viongozi wa mkoa wa Kilimanjarao
na Halmashauri ya Hai, Moshi kwa kutoa watumishi wa ziada ili kuongeza
nguvu.
Amesema kuwa abiria kuchelewa kumaliza hatua za vipimo vya
afya pia inachangiwa na baadhi yao kutojaza taarifa zao za hali yao ya
afya kupitia mfumo wa kieletroniki wa afyamsafiri ambao unamtaka abiria
kujaza taarifa zake ndani ya masaa 24 kabla ya kuingia nchini na hivyo
kuwafanya wachelewe kuanza hatua ya uchunguzi wa awali (primary
screening) na mwisho kufanya hatua zote za kulipia na kupima kuchelewa
pia.
Aidha, ametoa wito kwa mashirika ya ndege na mamlaka ya
viwanja vya ndege, usafiri wa ndege na wakala wa ndege, mabasi
kushirikiana kutoa elimu ili taarifa hizo zijazwe mapema kabla ya kufika
katika maeneo yetu ya viwanja vya ndege, bandari na mipaka yote.
Kwa
upande wa vipimo vya awali ameelekeza ufanyike utaratibu wa kuongeza
idadi ya wapimaji kutoka watano hadi kufikia 8 na wakati huo uratibu
ufanyike kuomba wahasibu kutoka wizara ya fedha kwa ajili ya kuratibu
malipo kwa ushirikiano na banki husika na wataalamu wa afya wahusike na
kuongeza nguvu ya kutoa huduma za afya.
Pia kwa kuzingatia
kuelekea msimu wa wageni wengi wizara itashirikiana na wadau wake
kuimarisha huduma za vipimo vya haraka huku ikiendelea kupokea maoni
mbalimbali na kuyafanyia kazi. Vilevile, amesema wizara itaendelea
kuboresha mfumo wa afyamsafiri ili uweze kurahisisha taratibu za
kuwahudumia wasafiri kabla hawajaanza safari na kupunguza changamoto
mbalimbali wanazolalamikia wakati wanapowasili nchini.
Waziri Dkt.Gwajima akimpima joto msafiri aliyewasili nchini ikiwa ni hatua za awali za uchunguzi wa Afya za wasafiri.
Eneo maalum la kupima kipimo Cha haraka Cha Covid-19 (Rapid Test) kilichopo ndani ya uwanja wa ndege wa KIA ambapo wasafiri wanaowasili nchini hupimwa kabla ya kuanza taratibu zingine ndani ya uwanja
Mmoja wa wataam wa Afya waliopo Kwenye vyumba maalumu vya kupima kipimo Cha haraka Cha Corona akipima kipimo Cha haraka Cha Corona kutoka kwa msafiri aliyewasili nchini.
No comments:
Post a Comment