HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 6, 2021

BENKI YA EQUITY (T) YAFUTURISHA ZANZIBAR

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh. Zubeir Ali Maulid ameipongeza Benki ya Equity kwa kutoa huduma nafuu zaidi nchini hivyo kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kupata huduma za kibenki. Akizungumza katika Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa Wateja wa Zanzibar, Spika Zubeir alisifu Benki ya Equity  kwa kuendesha akaunti  zake bila makato ya mwezi hivyo kutoa unafuu kwa wananchi.

 'Napongeza sana wazo lenu la kuondoa makato ya mwezi na kupunguza gharama za uendeshaji wa akaunti zenu kwani linatoa ahueni kwa wananchi wengi zaidi kutumia fursa za benki. Hongereni sana" alisema.

Spika  Maulid pia alishukuru Benki ya Equity kwa kuandaa futari kwa wateja wake ili kuungana nao katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. “Tunawashukuru Benki ya Equity kwa kuona umuhimu wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja wake ili kuweza kuwakutanisha pamoja na kuweza kuwatambua kwa lengo la kukuza umoja na mshikamano.

 Hili ni jambo la Faraja sana. Endeleeni kuwa karibu na Wateja wenu na muwafungulie milango ya uwezeshaji kiuchumi" alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mikopo, Ramadhan Chakinja, alisema kuwa  Benki ya Equity wamefarijika kutoa sadaka ya futari hiyo kama sehemu ya kuunga mkono waumini wa dini ya Kiislamu nchini. "Benki ya Equity imejiwekea utaratibu  kila mwaka kushiriki katika futari na wateja wetu kwa lengo la kuomba dua pamoja na na kuomba yaliyo mema.Tunathamini jumuiya ya Waislamu na tutaendelea kuwa nao bega kwa bega,” alisema.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh. Zubeir Ally Maulid akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Benki ya Equity (T) kwa wateja wake wa Zanzibar katika hoteli ya Medinat AL Bahar Mjini Unguja jana. 
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya Equity(T) Ramadhan Chakinja, akitoa salaam kwa Wateja wa Benki ya Equity Zanzibar katika Iftar ya Benki hiyo.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad