TAWA , CHUO KIKUU CHA UDSM WAZINDUA MAGOFU MARATHON KILWA LENGO NI KUTANGAZA UTALII WA WILAYA YA KILWA NA MKOA WA LINDI.
Na John Nditi, Kilwa
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamezindua na kuanzisha rasmi mashindano ya Magofu Marathon ya Kilwa , mkoani Lindi yatakayokuwa yakifanyika kila mwaka mwanzo wa mwezi wa Aprili yakiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa malikale , fukwe ,magofu na viumbe vya chini ya bahari.
Mashindano hayo ya mara ya kwanza yalizunduliwa Mjini Kilwa Masoko na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi , aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa mkoa huo, Rehema Madenge ,ambapo pia wakiwemo na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tawa iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko .
Mbio hizo za ridhaa zilikuwa za kilometa tano, Kilometa 10 na Kilometa 21 na kushirikisha wanariadha kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam, Tawa , Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kilwa , Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Lindi na kubeba kauli mbiu ya “ Tukimbie , Kutunza Urithi wetu”.
Mashindano yao yaliyoshirikisha mamia ya wanariadha ambapo Mratibu wake kutoka Chuo Kikuu UDSM ,Dk Elgidius Ichumbaki , aliwataja washindi wa mbio za kilometa tano wa kwanza alikuwa Mwajuma Kiluvia aliyetumia dakika 59: 44, mshindi wa pili ni Tukemelile Mgaya (59: 45) na watatu ni Ibrahim Khalfan (59:52).
Kwa upande wa mbio za kilometa 10 mshindi wa kwanza alikuwa ni Azilu Kiumjile (73:10), wapili ni Joseph Chiza (73: 45), na watatu ni Jacob Machesa (74: 30) .
Katika mbio za kilombeta 21 mshindi wa kwanza alikuwa ni Zishi Imran (93: 10), mshindi wa pili ni Sudi Said (95: 50) na mshindi wa tatu ni Semedo Athuman (99:10).
Washindi hao walipewa cheti na ngao kwa kutambuliwa kwo , huku wengine walioshiriki walipatiwa medali za kutambua mchango wao wa ushiriki na majina yao kuandikwa kuwa ni waanzilishi wa mashindano hayo.
Wengine walioshiriki na kuunga mkono kuanzishwa kwa Magofu Marathon kwa kukimbia umbali wa kilometa tano ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Tawa , Meja Jenerali Mstaafu Semfuko ,Naibu Kamishna wa Huduma za Utalii na Biashara wa Tawa , Imani Nkuwi ,Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Udsm , Profesa William Anangasye.
Wakimbiaji wengine walikuwa ni Katibu Tawala wa mko wa Lindi , Rehema Madenge pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kilwa ,Christopher Ngubiagai ambaye ndiye ni chachu kuweza kuanzishwa mwa Magofu ya Marathon ya Kilwa kwa lengo la kukuza na kutangaza utalii wa eneo la wilaya ya Kilwa na mkoa wa Lindi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko akimkabidhi mmoja wa washindi wa mashindano ya Magofu Marathon ya Kilwa ambayo yaliandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Mamlaka hiyo ,mjini Kilwa Masoko na yalibeba kauli mbiu ya “ Tukimbie , Kutunza Urithi wetu” na yatafanyika kila mwaka mwanzo wa mwezi wa Aprili yakiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa malikale , fukwe ,magofu na viumbe vya chini ya bahari.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Magofu Marathon ya Kilwa wakifurahia kupata medali zao za ushiriki wao kwenye mashindano yaliyofanyika katika Mji wa Kilwa Masoko , wilayani Kilwa , mkoa wa Lindi , ambayo yalibeba kauli mbiu ya “ Tukimbie , Kutunza Urithi wetu”na yatakuwa yakifanyika kila mwaka mwanzo wa mwezi wa Aprili yakiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa malikale , fukwe ,magofu na viumbe vya chini ya bahari.( Picha na John Nditi).
No comments:
Post a Comment