HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 6, 2021

RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA KAMPUNI YA MASTERLIFE MICROFINANCE LTD

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, akitowa taarifa ya Serikali kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, iliyokuwa ikiendesha shughuli za kifedha ikiwemo kupokea amana na kutoa mikopo kinyume cha Sheria na taratibu za Nchi, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 6/4/2021.

MWANDISHI wa habari wa ITV Ndg. Farouk Karim akiuliza maswali wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akitowa taarifa ya Serikali kwa Waandishi wa habari kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, ilioko Zanzibar, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
MWANDISHI wa habari wa gazeti la Dailynews Zanzibar Ndg. Masato Masato akiuliza swali kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kutoa taarifa ya Serikali kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
MWANDISHI wa habari wa Gazeti la Zanzibar leo Bi. Mwantanga Ame akiuliza swali wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akitowa taarifa wa Serikali kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, iliyokuwa ikitowa huduma za Kifedha, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
WAANDISHI wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani ) akitowa taarifa ya Serikali kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, ilikuwa ikiendesha shughuli za kifedha kinyume na sheria, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad