Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
WAZIRI
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewahakikishia
wafanyabiashara hapa nchini kuwa Wizara yake itahakikisha inarejesha
taswira na mahusiano mazuri nao katika masuala yakodi ili kuboresha
mazingira ya ufanyaji biashara na kusisimua uchumi wa nchi.
Dkt.
Nchemba alitoa ahadi hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam alipozungumza na
vyombo vya habari baada ya tukio la kuapishwa kwa Makatibu Wakuu na
Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wa Taasisi, tukio lililofanywa
na Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
“Tutatengeneza
vyanzo vipya vya makusanyo ili mzigo wa kodi usibebwe na wachache kwa
sababu kadri mzigo unavyobebwa na wengi ndivyo nafuu inavyopatikana,
hatua itakayowafanya wafanyabiashara wengi kulipa kodi kwa hiari”
alieleza Dkt. Nchemba
Aidha, Dkt. Nchemba aliyeanza kazi hivi
karibuni kama Waziri wa Fedha na Mipango, alisema kuwa amekutana na
wataalam wa Wizara yake na kuwaagiza wakutane na wenzao wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar ili kujadili namna ya kutatua changamoto za Muungano
na kwamba anaamini zitapatiwa ufumbuzi.
“Shida ya watu wetu wengi
wanapojadili masuala haya hawatuambii walipokwama, kwahiyo niliwaambia
watubainishie wanapokwama ili tupate ufumbuzi wa jambo hilo baada ya
hapo tutakaa Wizara tatu, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Fedha na
Mipango Zanzibar na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanya uchambuzi wa
kina” Alifafanua Dk. Nchemba
Kuhusu udhibiti wa matumizi wa Fedha
za Umma, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa Wizara yake itatumia
mifumo ya fedha iliyobuniwa kudhibiti matumizi ya Serikali na kuboresha
mifumo ya ukusanyaji wa mapato ili iwe michache lakini yenye ufanisi
pamoja na kuimarisha masuala ya utawala katika kukusanya mapato na
matumizi yake ili fedha hizo zilete matokeo yaliyokusudiwa.
Waziri
wa Fedha na Mipango alishuhudia kuapishwa kwa watendaji wake wapya,
akiwemo Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu ambao wameapishwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mher. Samia Suluhu Hassan,
Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Tuesday, April 6, 2021
DKT. NCHEMBA: TUTABORESHA MASUALA YA KODI NA KUSIMAMIA MATUMIZI YA SERIKALI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment