WATENDAJI WIZARA YA MALIASILI WAKAGUA VIJIJI VILIVYOVAMIWA NA TEMBO VILIVYOKO KWENYE USHOROBA MAKUYUNI MKOANI ARUSHA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 16, 2021

WATENDAJI WIZARA YA MALIASILI WAKAGUA VIJIJI VILIVYOVAMIWA NA TEMBO VILIVYOKO KWENYE USHOROBA MAKUYUNI MKOANI ARUSHA

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. ACP Edward Balele akizungumza na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wataalam kutoka TAWA, TANAPA na TAWIRI kuhusu namna ya kutatua changamoto ya uvamizi wa tembo kwenye eneo la ushorobo la vijiji vya Makuyuni, Wilayani Monduli katika kikao kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. ACP Edward Balele (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wataalam kutoka TAWA, TANAPA na TAWIRI baada ya kikao kilichozungumzia namna ya kutatua changamoto ya uvamizi wa tembo kwenye eneo la ushorobo la vijiji vya Makuyuni, Wilayani Monduli kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. ACP Edward Balele (katikati) akiteta jambo na Afisa Wanyamapori  Mkuu, Pellage Kauzeni (kulia) ambaye pia ni Kiongozi wa Msafara kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kikao kilichohusu namna ya kutatua changamoto ya uvamizi wa tembo kwenye eneo la ushorobo la vijiji vya Makuyuni, Wilayani Monduli kilichofanyika leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli. Kushoto ni Afisa Wanyamapori Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii , Antonia Raphael.
Baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakiongozwa Afisa Wanyamapori  Mkuu, Pellage Kauzeni (kushoto) na wataalam kutoka TAWA, TANAPA na TAWIRI, wakikagua moja ya shamba lililovamiwa na tembo katika kitongoji cha Lemioni, Makuyuni Wilaya ya Monduli leo.
Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Silvanus Okudo akionyesha namna tembo alivyofanya uharibifu katika kijiji cha Naiti, Makuyuni, Wilaya ya Monduli leo. Wanaoshuhudia ni Afisa Wanyamapori Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii , Antonia Raphael (wa pili kutoka kulia) na Mtafiti Mwandamizi kutoka TAWIRI, Hamza Kija (kushoto).

Mtafiti Mwandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Chediel  Mrisha akiteta jambo na Mtafiti Mwandamizi kutoka TAWIRI, Hamza Kija (kushoto) katika ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yaliyovamiwa na tembo yaliyoko Makuyuni, Wilaya ya Monduli.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad