HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 16, 2021

AFISA UHAMIAJI BABATI AHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA KWA RUSHWA

 

Na Mwandishi wetu, Babati

Afisa uhamiaji wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Silvester Jacob Kayani amehukumiwa kifungo cha miezi mtatu kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kupokea rushwa ya shilingi laki moja.

 Afisa huyo Kayani amepatikana na hatia hiyo hivyo kuhukumiwa kwenda jela miezi mitatu au kulipa faini ya shilingi laki sita ambayo alishindwa kuilipa na kupelekwa gereza la Mrara kutumikia kifungo hicho.

 Hakimu wa mahakama  ya Wilaya ya Babati Victor Kimario ametoa hukumu hiyo jana baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Martin Makani na Evelyine Onditi.

Afisa uhamiaji huyo Kayani alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 26 mwaka 2020 na kupatikana na hatia na kupelekwa gerezani baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi laki sita.

Awali, Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu amesema walipokea taarifa kutoka kwa mwananchi mkazi wa Babati na mzaliwa wa Singida kuwa anadaiwa rushwa ya shilingi laki moja na afisa uhamiaji huyo Kayani.

Makungu amesema afisa uhamiaji huyo Kayani alitaka fedha hizo ili asimchukulie hatua kutokana na tuhuma za uhamiaji haramu alizokuwa amezipokea dhidi ya raia huyo.

“Tulifanya uchunguzi na kubaini mlalaikaji huyo alikuwa mzaliwa wa Singida, baba na mama yake ni watanzania wa kuzaliwa ikiwa ni pamoja na uzao wao wote uraia wao wa kuzaliwa siyo wa kutiwa shaka hata kidogo, amesema Makungu.  

Amesema mtego wa rushwa uliandaliwa ulisababisha kukamatwa kwa afisa uhamiaji huyo kwenye hoteli iitwayo Royal Beach iliyopo karibu kabisa na ziwa Babati.

“TAKUKURU Mkoani Manyara tunawakumbusha waajiri wote wa utumishi wa umma kuwa kanuni ya 50 (e) ya kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003 zinaelekeza kuwa mtumishi wa umma akipatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani kama alivyopatikana Kayani kwa makosa ya kinidhamu na hivyo hatua za kumuondoa kwenye utumishi wa umma hufanyika,” amesema.

 “Aidha kanuni F.39 (3) ya kanuni za kudumu za utumishi wa umma za mwaka 2009 zinaeleza wazi kwamba mtumishi wa umma yeyote atakayepatikana na hatia ya makosa ya jinai yanayohusisha vitendo vya rushwa au ubadhirifu wa fedha na mali ya umma, mtumishiwa namna hii atapoteza haki zake zote au madai yake yote ndanin ya utumishi wa umma,” amesema Makungu.

 Ametoa rai kwa mamlaka zote za nidhani mkoani Manyara, ambazo watumishi wake wamekwisha kupatikana na hatia mahakamani kwa makosa yaliyoainishwa katika sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007, wachukue hatua za kuwaondoa watumishi wa aina hiyo kama sheria ya utumishi wa umma na kanuni zake inavyoeleza.

“Kwa mamlaka ya nidhamu tutakayokuta inamlinda mtumishi wa aina hii basi wafahamu kuwa sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma na tutaanza kuchukua hatua kwa mamlaka za nidhamu kwa kuwafungulia mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi,” amesema Makungu.

 “Aidha tunatoa muda hadi kufikia Aprili 15 mwaka huu mamlaka za nidhamu mkoani Manyara, ziwe zimetekeleza maelekezo ya kuwaondoa kwenye utumishi wale wote waliopatikana na hatia za makosa ya rushwa ambayo kipindi cha kukata rufaa kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jiana (CPA.1985) kilishapita.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati.

 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad