HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 12, 2021

TANGA UWASA YAUNGANISHA BOMBA KUBWA ENEO MOWE LITAKAPOLEKEA MAJI WILAYANI MUHEZA

MKURUGENZI wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) Mhandisi Geofrey Hilly (aliyevaa kofia)  kushoto akiangalia namna kazi inavyoendelea ya kushusha bomba kubwa ambalo linaunganishwa eneo la Mowe na kupelekea maji wilayani Muheza  
Mafundi wakiendelea na kazi kama wanavyoonekana kwa ajili ya kuuangisha Bomba kubwa la Maji
Greda likiendelea na shughuli zake kama linavyoonekana

Msimamizi wa Mradi Mkubwa wa Kupeleka Maji Muheza kutoka eneo la kutibu maji la Mowe,Mhandisi Salum Ngumbi kushoto akiteta jambo nMhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Peritach SB Limited ,Teobadi Nyalu katika anayefuatilia ni Afisa Uhusiano wa Tanga UWASA Devotha Mayala

MKURUGENZI wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) Mhandisi Geofrey Hilly wa tatu kutoka kushoto akiwa na watumishi wa mamlaka hiyo wakiangalia namna shughluli zinazovyoendelea

 

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) imeunganisha bomba kubwa la maji ambalo litakuwa likitoa maji kwenye mtambo wa kutibu maji wa Mowe uliopo eneo la Pande Jijini Tanga mpaka eneo la Kilapula ambayo yatakuwa yakisukumwa kuelekea wilayani Muheza ili kuondosha adha ya maji wilayani humo.

Akizungumza wakati wa zoezi la uunganishaji wa Bomba hilo Afisa Uhusiano wa Mamlaka la Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) Devotha Mayala alisema maji hayo yatakapofika eneo la Kilapula yatakuwa yakisukumwa kuelekea wilayani Muheza.

Devotha alisema wanatekeleza shughuli hizo ili kuhakikisha maji yanapatikana kwa wakati tofauti na awali ambapo maji yalikuwa yakipatikana kwa mgao wa mara tatu kwa wiki tu, huku akiekeza pia wananchi wa Pongwe nao watanufaika na mradi huo kutokana na kwamba hali ya huduma itaimarika na maji yapatikana masa 24 na wao kama taasisi wataendelea kutekeleza miradi mbalimbali kuhakikisha wanaondosha kero ya maji

Alisema tokea walipokabidhiwa wilaya ya Muheza wananchi walikuwa wanapata maji kwa asilimia 35 kwa mgao mara tatu kwa wiki na wanachofanya mwakia huu kama taasisi ni kutekeleza miradi ya kuboresha huduma kwenye maeneo yao mapya ya Muheza na wilaya ya Pangani.

“Kuna mradi ambao unakwenda ukingoni wa kuboresha huduma ya maji Muheza tulikwisha kujenga Tanki la Kuhifadhi Maji eneo la Kilapura na Pump House ambapo tunaamini kwamba tatizo la maji Muheza litakuwa historia “Alisema Afisa Uhusiano huyo.

 Awali akizungumza wakati wa utekelezaji wa shughuli hizo Msimamizi wa Mradi Mkubwa wa Kupeleka Maji Muheza kutoka eneo la kutibu maji la Mowe,Mhandisi Salum Ngumbi alisema kuwa kazi walionayo ni kuunganisha toleo kubwa la bomba la milimita 300 ambayo ni hatua muhimu ya kupelekea maji wilayani Muheza.

Mhandisi Salum alisema litakapokamilika litawezesha wananchi wa wilaya ya Muheza kupata maji masaa ya 24 na kuondoa mgao huku akieleza pia hali hiyo itasaidia maeneo ya Muheza na Pongwe kupata maji masaa 24 na hivyo wananchi kuondokana na adha ya kusaka huduma hiyo mbali .

Alisema kwamba mradi huo ulianza mwezi May mwaka 2019 na unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji na una thamani ya shilingi ubilioni 2.6 ukiwa na lengo la kuwanufaisha wananchi elfu 15000 wanaoishi mji wa muheza na wananchi 8000 wanaosihi kwenye Vijiji vya Njiani kutokea Tanga kwenda Muheza.

“Kukamilika kwa mradi huu utaongoza hali ya upatikanaji wa mji wa Muheza kutoka asilimia 35 ya sasa mpaka kufikia 64 wananchi wa muheza watapata maji siku saba za wiki na hivyo itawaondolea adha ambazo walikuwa wakikumbana nazo awali”Alisema

Naye kwa upande wake,Mhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Peritach SB Limited ,Teobadi Nyalu alisema mradi huo walikabidhiwa May 30 mwaka 2019 wa bomba lenye ukubwa wa milimita 300 na kulazma bomba kutoka Mowe hadi Pongwe kilomita 8.2 ambapo kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za utekelezaji wa mradi.

Alisema mpaka sasa wamekwisha kujenga chemba 20 na ufungaji wa vifaa mbalimbali ili kuwezesha wananchi kupata huduma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad