Mkuu
wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius
Gambosi (aliyenyoosha mikono na kushika fimbo) akitoa maelezo mafupi
jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) kuhusu zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Mkuu
wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius
Gambosi (aliyenyoosha mikono na kushika fimbo) akitoa maelezo mafupi
jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) kuhusu zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi (aliyeshika fimbo) akimuongoza jana kwa Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti)
kuelekea eneo mojawapo la zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa
likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa
siku saba.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) akisalimiana jana na Maafisa wa Jeshi la Wananchi kutoka Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi alipohudhuria kusitisha kwa zoezi la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi akimkabidhi jana kwa Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) Bendera
ikiwa ni ishara ya kumalizika kwa zoezi la utangulizi la kijeshi
lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa
Isawima kwa siku saba.
Mkuu wa Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi akimuonyesha jana kwa Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) mmoja
ya mabomu ambayo walikuwa wakiyatumia katia zoezi la utangulizi la
kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya
Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Wapiganaji Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi, wakilipua mabomu jana wakati wa zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Mkuu wa
Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( mwenye suti ya drafti) akiangalia
mmoja mzinga wa kurusha mamomu wakati wa kuhitimisha zoezi la
utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika
ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Mkuu
waMkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati( katikati mwenye suti ya drafti)
akishiriki mazoezi jana na Maafisa wa Majeshi na Wapiganaji kutoka
Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi kabla ya kumalizika
kwa zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho uwezo
lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Wapiganaji kutoka Kamandi ya Brigedi ya 202 kundi la vikosi wakirudi katika eneo la Kambi ya muda baada ya kumalizika
jana kwa zoezi la utangulizi la kijeshi lililokuwa likijulikana onesho
uwezo lililofanyika ndani ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Picha na Tiganya Vincent
NA TIGANYA VINCENT
VIKUNDI vya watu
waliovamia na kubaki katika eneo
la Hifadhi ya
Wanyamapori ya Isawima lilipo wilayani Kaliua ambao wanaendelea kuendesha
shughuli za kilimo na ufugaji wametakiwa kuondoka kwa hiari kabla hatua
za kisheria hazijachukuliwa dhidi.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati akihitimisha zoezi
la utangulizi la kijeshi lililo kuwa likijulikana onesho uwezo lililofanyika ndani
ya Msitu wa Isawima kwa siku saba.
Alisema Serikali
imeamua kuchukua hatua baada ya kuona kuwa uvamizi katika eneo hilo unaendelea
na kutishia uendelevu wa ziwa Tanganyika na kupoteza maisha ya baadhi ya wananchi
na watendaji.
Mkuu huyo wa Mkoa
alisema Serikali haiwezi kuendelea kuwacha wavamizi waendelee la uharibifu
ambao utaishia ikojia ya eneo hilo ambalo ni muhimu kwa ajili ya upelekaji wa
maji ziwa Tanganyika na mapito ya wanyama kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Mto
Ugalla, Mbuga ya Kigosi Moyosi na Mpanda line.
Alisema Serikali ya
Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Kaliua wametumia Diplomasia na kutoa elimu ya
kutosha kilichobaki watu wote waliomo katika msitu kuondoa wao wenyewe kwa
hiari yao.
Dkt. Sengati aliwataka Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuhakikisha baada bya kazi iliyofanywa na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania katika eneo wavamizi wasiingie tena na kuharibu maliasi ikiwemo ukataji magogo
na uwindaji haramu wa wanyamapori unaofanyika katika eneo hilo.
Aliwataka
kufanyakazi kwa kuzingatia maadili na sharia katika kuhakikisha wavamizi wote
na vikundi vyote vya uhalifu vilivyomo ndani ya msitu huo vinaondoka ili
uharibifu usiendelee.
Alisema lengo la
Serikali ni kutaka msitu huo hatimaye uje upande kwa ajili ya kuongeza mapato
ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na Taifa kwa ujumla.
Naye Mkuu wa Kamandi ya
Brigedi ya 202 kundi la vikosi, Brigedia Jenerali Julius Gambosi alisema zoezi
hilo ni utangulizi wa zoezi kubwa litakalofanyika katika Hifadhi hiyo limekuwa
na mafanikio makubwa ambalo limewaongezea uwezo na ujuzi wapiganaji.
Alisema kuwa lengo la
zoezi hilo ilikuwa ni maandalizi ya zoezi kuwa litakalofanyika katika Hifadhi
hiyo hivi karibuni ikiwa ni kuwaweka Makanda kuwa tayari wakati wowote kuliinda
Tanzania dhidi ya uchokozi wowote.
Brigedia Jenerali
Gambosi alisema zoezi hilo lilinakuja litakuwa la kiwango cha juu.
Aidha alisema kuwa eneo
hilo ni muhimu kuhakiisha hakuna wavamizi ndani na kuiomba Serikali kuendelea
kutoa elimu kwa watu waliomo ndani yake ili waweze kuondoka kwa hiari kwa ajili
ya kulitunza na kuendeleza hifadhi kwa matumizi endelevu ambayo yatakuwa na
manufaa kwa wananchi wengi.
Alisema kuendelea
kuwaacha wavamizi ndani ya Hifadhi hiyo kunaweza kusababisha hata vikundi vya
kiharifu kujificha ndani yake.
No comments:
Post a Comment