Kaimu
Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (kushoto) akifungua
pazia kuashiria uzinduzi wa jengo la Utawala la Shule ya Awali na Msingi
ya Genezareth iliyopo Manispaa ya Singida mwishoni mwa wiki. Kulia ni
Meneja wa shule hiyo, Sister Yohana Duwe.
Katibu wa Elimu wa Jimbo Katoliki Singida, Padri Gilbert Mwiru akizungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (kushoto) akitoa zawadi kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiimba katika hafla hiyo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiimba katika hafla hiyo.
Kaimu
Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (kushoto) akitoa
zawadi.kwa mmoja wa wanafunzi aliyefanya vizuri mtihani wa darasa la
nne.
Jengo la chakula lililo zinduliwa.
Jengo la Utawala lililo zinduliwa.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KAIMU Afisa Vijana mkoani hapa Frederick Ndahani amewataka walimu na walezi kuwa lea watoto katika maadili ya kizalendo.
Ndahani
ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt.Rehema Nchimbi alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwenye hafla ya
uzinduzi wa majengo matatu ya Shule ya Awali na Msingi ya Genezareth
iliyopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida.
"
Tukiwa na Taifa la wasomi na wazalendo tutaisogeza nchi yetu kwenye
uchumi wa juu hivyo ni jukumu la walimu na walezi kuwafundisha watoto
wetu maadili ya uzalendo kuanzia shule za awali na kuendelea." alisema
Ndahani.
Ndahani
alisema anasikitika kuona vijana waliosomeshwa na Serikali ndio
wanakuwa mstari wa mbele kupinga mambo ya maendeleo yanayofanyika hapa
nchini kutokana na kukosa uzalendo.
Aidha
Ndahani alitumia nafasi hiyo kuomba elimu ya kujitegemea ianze kutolewa
mashuleni pamoja na kuanzisha miradi itakayo wajenga wanafunzi kiuchumi
kuanzia ngazi ya chini.
Katibu
wa Elimu wa Jimbo Katoliki Singida, Padri Gilbert Mwiru aliishikuru
Serikali kwa kushirikiana na mashirika ya dini kwa ajili ya kuwaletea
maendeleo wananchi na kueleza kuwa katika Mkoa wa Singida jimbo hilo
lina taasisi za elimu 23, shule za msingi 10, Sekondari 8 na vyuo vya
kati 5.
Meneja
wa shule hiyo ambayo inamikiwa na Jimbo Katoliki Singida, Sister Yohana
Duwe alisema majengo yaliyozinduliwa ni jengo la Utawala, Bweni na
Bwalo la chakula na kuwa ujenzi huo umegharimu zaidi ya Sh.milioni 3000.
Sister
Duwe alitumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kusaidia kuboresha
miundombinu ya umeme na maji ambayo haipo na kueleza kuwa hivi sasa
wanatumia umeme wa jua (sola) pamoja na maji ya mvua ambayo hayakidhi
mahitaji.
No comments:
Post a Comment