Na Mwandishi wetu, Simanjiro
WANAFUNZI 24 yatima wa shule ya msingi Songambele Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wamenufaika na sare za shule baada ya Katibu wa chama cha wachimbaji madini Mkoani Manyara (Marema) Tawi la Mirerani Rachel Njau kuwapa msaada huo.
Njau ambaye pia ni Mjumbe wa chama cha wachimbaji madini wanawake (Tawoma) amekabidhi msaada huo kwa Diwani wa kata ya Mirerani, Salome Mnyawi.
Njau amesema sare hizo za wanafunzi hao 24 wasichana na wavulana ambao ni yatima zimejumuisha mashati, kaptula, sketi, nguo za ndani, soksi na viatu.
Amesema wamewezesha msaada huo akishirikiana na mtanzania anayeishi nchini Marekani, Hannah Jenge Kamau ndipo wakanunua sare hizo za shule.
"Nilikutana na Diwani wa kata ya Mirerani, Salome Mnyawi akanieleza changamoto za watoto hao yatima nami nikamshirikisha mdau wangu wa maendeleo, Hannah Jenge Kamau ndipo tukafanikisha haya kwa ajili ya watoto hawa yatima ili nao wajisikie kuwa wana wazazi." Amesema Njau.
Amesema yeye huwa anakawaida wa kuwa na moyo wa kutoa na siyo mara yake ya kwanza kwani ameshawezesha misaada mbalimbali hivyo akawiwa kuwasaidia watoto hao yatima 24 wa shule hiyo.
Diwani wa kata ya Mirerani Salome Mnyawi amewashukuru wadau hao wa maendeleo kwa kuwawezesha watoto hao yatima 24 sare hizo za shule.
"Hivi sasa watoto Hawa watasoma kwa bidii baada ya kupata sare hizo, nawashukuru sana wadau wangu Rachel Njau na Hannah Jenge Kamau kwa misaada yao kwa watoto hawa, wadau wengine wa maendeleo waige jambo hili." Amesema Salome.
Mkazi wa kata ya Mirerani, Deshifose Solomon amempongeza Rachel Njau kwa kusimama kidete hadi kufanikisha tukio hilo la watoto hao yatima 24 kupata sare hizo.
"Rachel Naju ana moyo wa huruma kwani naye ni mama mwenye uchungu na watoto wake tunamshukuru sana kwa tukio hilo kwa kuwasaidia watoto wetu." Amesema Solomon.
No comments:
Post a Comment