MATUKIO KATIKA PICHA: TUKIO LA KUUNGUA MOTO LA CHAAZ PUB - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 5 March 2021

MATUKIO KATIKA PICHA: TUKIO LA KUUNGUA MOTO LA CHAAZ PUB

Leo Ijumaa Machi 05, 2021 moto mkubwa ambao chanzo chake hakikufahamika mara moja, umeteketeza bar maarufu ya La Chaz Pub iliyopo eneo la Sinza Mori Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam.

Moto huo ulianza majira ya saa 9 alasiri uliteketeza eneo kubwa na bar hiyo kabla ya Jeshi la zimamoto na uokoaji kufika na kufanikiwa kuzima moto huo.

Akielezea chanzo cha moto Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Ilala, Ndg. Elimino Shang'a  amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na wanaendelea na uchunguzi, kuhusu thamani ya vitu vilivyoungua, taarifa rasmi itatolewa baadae. Picha na SamTiger, MichuziTV

Endelea kufuatilia Michuzi TV Updates kwa taarifa za papo hapo.

Sehemu ya La Chaaz Pub inavyoonekana sasa baada ya kuteketea kwa moto huo.

Askari Polisi wakiendelea kusimamia ulinzi eneo la tukio. #ChaguaKupambana

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad