.
Katika kuazimisha siku ya wanawake duniani, kampuni ya Halotel Tanzania
imesherekea kwa kuunga mkono juhudi za wanawake katika majukumu yao ya
kujikomboa kiuchumi na kujenga taifa kiujumla.
Kutokana na ukweli
kwamba wanawake wamekuwa wadau na mstari wa mbele katika kujikwamua
kiuchumi, kifikra na kusaidia jamii, Kampuni ya simu ya Halotel
imethamini jitihada hizo kwa kutoa msaada wa hali na mali kwa wanawake
hawa ikiwa ni katika kutambua juhudi zao kubwa kwa namna mbalimbali.
Halotel
imetoa mifuko hamsini (50) ya chakula na malazi kwa wakina mama 50
katika soko la Mwananyamala jijini Dar es salaam, ikiwa ni zawadi kwa
wakina mama hawa wanaopambana kila siku kujitafutia riziki. Zawadi hizo
ziliwasilishwa na wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Halotel kama moja
wapo ya namna ya ya kusherekea siku ya wanawake duniani.
Akitoa
ufafanuzi katika zoezi la kukabidhi zawadi hizo kwa wanawake katika Soko
la Mapinduzi lililoko Mwananyamala Mkuu wa Idara ya Masoko Halotel
Sakina Makabu alisema "wanawake wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii
ili kuboresha hali zao za kiuchumi na kusaidia jamii, kama Halotel,
tunathamini na kutambua juhudi zao kwa kile wanachofanya na kutoa msaada
kwao.”
‘Tunafurahi kusherekea na wanawake wenzetu kwa kutoa
zawadi za mahitaji ya nyumbani lakini pia kupata wasaha wa kubadilishana
mawazo’ aliongeza Sakina.
Halotel imewashukuru wanawake wote
ambao wamekuwa wakipambana katika kuikwamia katika Nyanja mbalimbali za
maisha na kuwapongeza katika kusheherekea siku ya kimataifa ya wanawake
Duniani.
Kampuni
ya simu ya Halotel imetoa zawadi kwa wanawake Hamsini (50) katika
kusheherekea siku ya wanawake Duniani. Wafanyakazi wanawake kutoka idara
mbalimbali Halotel walishiriki kutoa zawadi za mahitaji ya nyumbani kwa
wanawake wajasiliamali katika Soko la Mapinduzi lililopo Mwananyamala
jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment