Shabiki wa klabu ya Simba na Liverpool Joel Mtalamu ameshinda Sh 78,265, 530 baada ya kubashiriki kwa usahihi zaidi matokeo ya michezo 12 ya mpira wa miguu ya ligi mbalimbali duniani kupitia droo ya Perfect 12.
Mtalamu ambaye ni mkazi wa Kidatu, Kilombero anakuwa mshindi wa nane wa droo hiyo tokea kuanza kwa mwaka huu kwa mujibu wa Meneja wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi.
Mushi alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa sana kuendelea kuwainua vipato Watanzania kupitia michezo yao ya kubahatisha. Washinda hao wanaingia katika orodha yao ya nyumba ya mabingwa.
“Ni faraja kwetu kuona Watanzania wengi wanashinda kupitia michezo yetu ya kubahatisha. Tutaendelea kuwa nyumba ya mabingwa huku tukiendelea kuwainua vipato vyao,” alisema Mushi.
Kwa upande wake, Mtalamu aliipongeza kampuni hiyo kwa kufanya shughuli zake kwa uwazi na kuwazawadia washindi. “Nimefarijika sana kushinda leo (Jana), hizi fedha nitaanzisha biashara mpya huku nikihimarisha biashara yangu,” alisema Mtalamu.
Wakati huo huo jumla ya washindi wanne wameshinda zawadi ya fedha katika mchezo mpya wa kubahatisha wa M-Bet unaotambulika kwa jina la Shinda Extra.
Washindi hao ni Daniel Mbasha, Hamisi , Victor na Jusiri Allem ambao kila mmoja amejishindia Sh500,000.
Kupitia mchezo huo, M-Bet itakuwa inatoa zawadi ya Sh500,000 kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa na Shmilioni 1 kwa siku za Jumamosi na Jumapili.
Mushi alisema kuwa kampuni hiyo itatumia si chini ya Sh18 millioni kuzawadia washindi kupitia mchezo huo. Alisema kuwa kwa wachezaji ambao wamejisajili kupitia app ya M-Bet watalipa Sh500 ambapo hawajasajiliwa watalipa sh1000.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-BET, Allen Mushi (kulia) akikabidhi mfano wa hundi mshindi wa mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12, Joel Mtaalamu kutoka Kidatu, Kilombero. Mtaam alishinda kiasi cha Sh 78,265, 530.
Mshindi wa Sh 78,265, 530 kupitia mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12 wa M-BET, Joel Mtalamu (kushoto) akizungumza wakati wa utambulisho wake. Pembeni ni Meneja Masoko wa M-BET Tanzania, Allen Mushi.
No comments:
Post a Comment