WAZIRI KUKUTANA NA WANAMUZIKI ZAIDI YA 500 ARUSHA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 16, 2021

WAZIRI KUKUTANA NA WANAMUZIKI ZAIDI YA 500 ARUSHA

 

Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.
Katibu Mkuu wa wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), , Stella Joel.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Dofa kutoka Karatu ambao wataimba wimbo maalumu kwenye kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale
WAZIRI wa Habari, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa anatarajiwa kukutana na wanamuziki zaidi 500 katika kongamano la fursa litakalofanyika Jumamosi Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.

Katika kongamano hilo baadhi ya wanamuziki watakabidhiwa kadi za bima ya afya ya Taifa (NHIF) na Bashungwa ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

"Wanamuziki watakao pata kadi hizo ni wale ambao wametimiza vigezo kama walivyoeleza Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Eric Kisanga na Katibu Mkuu wa umoja huo, Stella Joel ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo.

Baadhi ya wanamuziki watakao kabidhiwa kadi hizo wametajwa kuwa ni mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Kida Waziri, Emmanuel Mbasha, Madamu Flora, Goodluck Gozibeth, Stara Thomas, Hafsa Kazinja Renatha Sedekia na Rehema Tajiri.

Akiwazungumzia Wanamuziki hao Katibu Mkuu wa TAMiUFO Stella Joel alisema wanaishukuru Serikali kwa kuwakumbuka kuwapatia kadi hizo ambazo zitawasaidia kupata vipimo na matibabu katika hospitali za Serikali na binafsi.

Joel alisema kabla ya hapo wanamuziki wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama za vipimo na matibabu.

" Kwa hatua hii iliyochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano hakika wanamuziki wote tunakila sababu ya kuipongeza kwa kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kutusaidia wasanii" alisema Joel.

Rais wa TAMUFO, Eric Kisanga alisema kongamano hilo ni la kipekee kwani litawahusisha wanamuziki wa kada zote na kuwa maandalizi yote yamekwisha kamilika.

" Maandalizi yote ya kongamano letu ili la fursa kwa wanamuziki yamekwisha kamilika kwa asilimia kubwa na sasa tupo kumalizia mambo madogo yaliyosalia" alisema Kisanga.

Kisanga alitumia fursa hiyo kuwakaribisha kwenye kongamano hilo wananchi, wasanii na wadau wengine wa muziki na kuwa halitakuwa na kiingilio ni bure.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad