HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 8, 2021

WATUMISHI TULINDE AFYA ZETU ILI TUWAHUDUMIE WANANCHI IPASAVYO – DKT.NDUMBARO

 

 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Watumishi wa ofisi yake leo jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi hao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akisisitiza jambo kwa Watumishi wa ofisi yake leo jijini Dodoma alipokutana nao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

……………………………………………………………………………………..

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, amewataka Watumishi wa Umma nchini kulinda afya zao ili waweze kuwahudumia vema wananchi wanaofuata huduma mbalimbali katika taasisi zao.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito huo mapema leo wakati akizungumza na Watumishi wa ofisi yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi hao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Dkt. Ndumbaro amesema, ili Watumishi wa Umma waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu, hawana budi kulinda afya zao ikizingatiwa kuwa  wakati wa utoaji huduma wanakutana na watu ambao baadhi yao wanaweza kuwa na changamoto mbalimbali za kiafya.

Ili kuhakikisha taifa linakuwa na rasilimaliwatu yenye tija, Dkt. Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara na kupata tiba mapema iwezekanavyo pindi wanapohisi kukabiliwa na changamoto yoyote ya kiafya.

Sanjali na hilo, Dkt. Ndumbaro amewahimiza Watumishi wa Umma kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya kwa lengo la kuendelea kutoa mchango katika ujenzi wa taifa. 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amekuwa na utaratibu wa kukutana na Watumishi wa Umma katika maeneo mbalimbali nchini kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad