HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 16, 2021

MAENDELEO BENKI YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA KAMPENI YA UPENDO WOTE KWAKO.

 

Tarehe 14 ya Mwezi wa pili kila mwaka watu husherekea siku hii ya Valentine kuketi na wapendwa wao kama ishara ya kuwaonesha mapenzi mazito waliyonayo juu yao, Maendeleo Bank kupitia kampeni yake ya Upendo Wote Kwako iliiishi tarehe 14/2/2021 kwa vitendo kwa kutimiza ahadi yake kwa wateja kwa kuwaandalia chakula cha usiku spesho kwa wateja wote washindi wa kampeni ya Upendo Wote Kwako.
Meneja Huduma kwa Wateja Bi. Sylvia Chaula akitoa neno la shukrani kwa washindi
Akizugumza katika hafla hii spesho kwaajili ya washindi Meneja Huduma kwa Wateja Bi. Sylvia Chaula alisema kiukweli mpambano ulikuwa mkali sana wateja wetu wameshiriki kikamilifu katika kuhakikisha wanapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kutoka Maendeleo Bank, lakini nilazima apatikane mshindi katika kila shindano. Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuwa nasi katika kila hatua na sisi ahadi yetu kwenu nikutowaangusha kila iitwapo leo tutakuja na majawabu ya kuhakikishaa dhama yetu ya kumsaidia kila mmoja wetu kujikwamua kiuchumi inakamilika kwani lengo letu kuu kama Benki ni kumuona kilamtanzania anakuwa na maisha bora huku akiwa na uwezo wakupata huduma zote bora za kifedha. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr. Ibrahim Mwangalaba
Tukio hili lilichagizwa na uwepo wa Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr. Ibrahim Mwangalaba ambaye ndie aliekuwa mgeni rasmi watukio zima la ugawaji zawadi wateja wetu wote ni washindini wapongeze wote walioshiriki katika kuweka na kutoa miamala yao kupitia MB Mobile pamoja na huduma za mitandao mingine ya simu kuweka fedha zao kwenye akaunti zao – alisisitiza Dr. Ibrahim Mwangalaba


Washindiwalioshindazawadihizini
1. DaimaYonaKinyunyu
2. Nelson Richard Wandwalo
3. Faitth Robert Massawe
4. Amoke Abraham Kyando
5. Ragegunda Patrick Temu
6. Mabbics Catering and Decoration
7. Gasto Colman Mrema
MkurugenziMtendaji Dr. Ibrahim Mwangalaba akiwa na washindi wote katika picha ya Pamoja Akiongea na vyombo vya habari mmoja wa washindi Ndg. Nelson Richard Wandwalo aliipongeza Maendeleo Bank kwa kuendelea kuwainua wafanyabiashara wadogo wadodgo na wa kati huku akishukuru kwa zawadi aliyoipata, Maendeleo Bank kwa kweli mmekuwa msaada mkubwa sana kwetu sisi wafanyabiashara, ninauchukua huu ushindi wangu nah ii simu niliyopata ninampatia Valentine wangu ambaye nimekuja nae hapa leo, Maendeleo Bank mnatuinua sana sana aliongeza Ndg. Nelson Richard

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad