RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA MAZIKO YA MAREHEMU MOHAMMED SEIF KHATIB - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 16, 2021

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA MAZIKO YA MAREHEMU MOHAMMED SEIF KHATIB

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Kiislam katika Sala ya kumuombea Marehemu Mohammed Seif Khatib ikiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, iliofanyika katika Masjid Noor Muhammad SAW kwa mchina mwazo na (kulia kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dk. Mohamed Ali Shein na (kushoto kwa Rais) Katibu Ofisi ya Mufti Mkuu Sheikh Abdalla Talib na Alhajj Balozi Seif Ali Iddi Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf, wakishiriki katika Sala ya kuusalia mwili wa marehemu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Mohammed Seif Khatib, wakati wa maziko yake yaliofanyika Kijijini kwao Umbuji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Waumini wa Kiislam wakiitikia dua baada ya kumaliza kwa Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Mohammeed Seif Khatib iliofanyika katika Masjid Noor Muhammad S.A.W kwa Mchina mwanzo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa marehemu Mohammed Seif Khatib ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman, iliofanyika katika Masjid Noor Muhammad S.A.W kwa mchina mwazo. na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein wakiitikia dua
Wananchi wakishiriki katika maziko ya marehemu Mohammed Seif Khatib yaliofanyika Kijijini kwao Umbuji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.leo 16-2-2021.
Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeka jeneza likiwa na mwili wa marehemu Mohammed Seif Khatib, wakielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya maziko yake yaliofanyika Kijijini kwao Umbuji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na waumini weningine wakiitikia dua ikisomwa na Sheikh Mohammed Kassim (hayupo pichani) (kulia kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaaf wa Zanzibar.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Balozi Seif Ali Iddi Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf na Mtoto wa Marehemu Seif Mohammed Seif.
Sheikh Mohammed Kassim akihitimisha kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea Marehemu Mohammed Seif Khatib iliofanyika katika Masjid Noor Muhammad S.A.W. Mombasa kwa Mchina mwanzo, kabla ya kuusalia mwili wa Marehemu.
(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad