HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 29, 2021

DMI YATAKIWA KUWA NA MELI YA MAFUNZO

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Suleiman Kakoso, akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo na Viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum, mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Mwanaisha Lulenge akitoa maoni yake wakati wa kikao cha kamati hiyo na Viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, jijini Dodoma.


KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha inakiwezesha Chuo cha Mabaharia cha Dar es Salaam (DMI), kununua meli ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho.

Hatua hiyo itakiwezesha chuo hicho kufanyakazi kazi zake kwa ufanisi na hivyo kutoa wahitimu wengi watakaokidhi soko la ajira la ndani na kimataifa.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Suleiman Kakoso, amesema kwa kuwa Chuo hicho kwa sasa kinahudumia wanafunzi kutoka nchi mbalimbali kama vile Uganda, Kenya, Rwanda na Zimbabwe kwa hiyo kikiwezeshwa kuwa na meli ya mafunzo kitapelekea wanafunzi wake kuwa na ujuzi wa kutosha wa mafunzo kwa vitendo na hivyo  kitafanikiwa kupata wanafunzi wengi kutoka nchi nyingine barani Afrika.

 Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Erick Masami, akiwasilisha taarifa ya Chuo hicho mbele ya kamati hiyo amesema Chuo hicho bado kinakabiliwa na upungufu wa majengo ya madarasa na ofisi.

Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Mwanaisha Lulenge amezungumzia umuhimu wa Taifa kuwekeza katika masomo ya ubaharia kwani wataalam wa fani hiyo hapa nchini bado ni wachache.

Naye, Naibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema Wizara imeyapokea na itayafanyia kazi mapendekezo yote ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ili kukiwezesha chuo cha mabaharia nchini kuwa kituo cha mafunzo cha umahiri katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad