HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 2, 2020

BENKI YA EQUITY YAFUNGUKA KIMATAIFA

Meneja wa huduma Mbadala za kibenki wa Euqity benki Bi. Magreth Mwasubi (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenzake wakionyesha mfano wa kadi zilizozinduliwa. Picha na Cathbert Kajuna wa MMG/Kajunason.

Na Mwandishi Wetu.

Equity Bank Limited, leo imezindua kadi mpya ya kisasa ya Visa inayotumia mfumo wa sarafu ya Dola ya Kimarekani ‘VISA USD Debit Card’ kwaajili ya matumizi ya wateja wake nchini Tanzania.

Kadi hiyo iliyotengenezwa kwa kiwango cha dhahabu ni ya kwanza na ya kipekee ikiwa na malengo ya kutoa urahisi na upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, ambao wanataka kufanya manunuzi kupitia mtandaoni au kufanya biashara kwa kutumia sarafu ya Dola ya Kimarekani. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Wanahabari Meneja wa huduma mbadaa za kibenki Magreth Mwasubi amesema kadi hiyo inampa mteja fursa ya kulipia bidhaa na huduma mbalimbali kwa sarafu ya Dola ya Kimarekani pasipo na nyongeza ya malipo yoyote ya ziada. Itamsaidia mteja kufanya miamala pasipo kuvuruga bajeti yake. 

 Meneja wa huduma mbadaa za kibenki Bi. Magreth Mwasubi amengeza kuwa kadi hiyo ni nafuu, inatoa suluhisho la bei, ni rahisi na salama kwa mteja na itamsaidia sana mteja katika kurahisisha huduma kwa wakati sahihi lakini pia kuchochea ukuaji wa biashara ya mtandaoni.

“Kadi ya Visa Gold Debit inaruhusu wateja kulipia bidhaa au huduma kwa Dola za Kimarekani kwa viwango vilivyoonyeshwa kwa wakati huo. Hii inamaanisha kuwa ikiwa unalipa bidhaa inayouzwa Dola 10 za Kimarekani, hiyo ndiyo inayokatwa katika akaunti yako- hakuna malipo mengine, ”anasema Magreth Mwasubi. 

Kwa upande wake Meneja huduma za kibenki Diaspora Bi. Doreen Raphael ameongeza kuwa VISA USD Debit Card inatumia mfumo wa PayWave ambapo pia mtumiaji ana uwezo wa kufanya manunuzi madogomadogo. 

Visa PayWave ni teknolojia ya malipo isiyohusisha mawasiliano ya moja kwa moja isipokuwa kupitia mawasiliano ya kimtandao kwa kutumia chip maalumu yenye ili mtumiaji kupokea malipo.

“Kadi hii inatumia mfumo wa chip na neno la siri kwaajili ya usalama na ubora kwa mtumiaji,” amesema Bi. Doreen Raphael.

Uzinduzi huo unakuja kufuatia mwenendo wa mabadiliko ya biashara ya kielektroniki, wakati ambao biashara nyingi zinahamia katika mtandao, ikiwa ni mojawapo ya madhara ya mlipuko wa Covid-19.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad