Na Baltazar Mashaka, Magu
MWENYEKITI
wa Kijiji cha Ijinga katika Wilaya ya Magu, Badri Juma Masengo (40)
anadaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya Msingi
Ijinga mwenye umri wa miaka 15 jina linahifadhiwa.
Kutokana
na kadhia hiyo jeshi la polisi Wilaya ya Magu,linamshikilia mwenyekiti
huyo kwa mahojiano akituhumiwa kutenda kosa hilo kabla ya kufikishwa
mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Akizungumzia
tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli alisema hakubaliani na
hatakubali kuona watoto wa kike wanakatishwa masomo na wanaume wenye
uchungu wa ngono wanaohangaika na wanafunzi ilhali wanawake wamejazana
mitaani na kuonya wenye tabia hiyo na watakaobainika atakula nao sahani
moja.
Alisema
katika wilaya hiyo yapo mambo ya ovyo yanafanywa na baadhi ya walimu,
wazazi na jamii kwa kufanya ngono na wanafunzi wa shule na kukatisha
ndoto zao za elimu na kuonya hatakubali hayo yaendelee na kutoa angalizo
kwa watumishi wa idara ya polisi na mahakama wanaopindisha sheria
sababu ya rushwa kwenye kadhia hiyo hawatabaki salama.
Kalli
alisema kuwa Rais John Magufuli amefuta ada kwa shule za msingi hadi
kidato cha nne na kurahisha mambo kwa wananchi ambao hawakuwa na uwezo
ili kuwawezesha watoto kusoma kwa raha watimize ndoto zao lakini watu
wachache kwa tamaa ya ngono wanawaharibia maisha.
“Ilani
ya uchaguziibara 80 inaeleza uboreshaji wa elimu kutoka msingi hadi
chuo kikuu mtoto asome hadi mwisho hata kama mzazi hana uwezo na
serikali inataka wasome kwa raha watimize ndoto zao na hivyo
sitawavumilia wanaume wanaojamiina na watoto na nitoe rai kwa idara ya
mahakama na polisi watende haki kwa mtoto aliyekatishwa masomo na
mwenyekiti huyo ili liwe fundisho kwa wengine wanaokiuka maadili na
kuharibu maisha ya watoto,”alisema.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema tatizo la rushwa kwa baadhi ya watumishi wa
mahakama na polisi wasio na uadilifu,linakwamisha juhudi za serikali na
kuwataka kuzingatia kauli ya Rais Magufuli wakati akimwapisha
Mwanasheria Mkuu.
“Jaji
Mkuu wa Tanzania naye alirudia maneno hayo,na mimi leo naelekeza sina
shaka na sitaki kuamini kuwa rushwa itatembea kwenye kesi hii,sitaki
kuhukumu maana ushahidi uko wazi, hivi mpepelezi katika kesi hii anataka
kueleza nini na ninaomba isichukue muda mrefu ili haki
itendeke,”alisema Kalli.
Mwanafunzi
huyo mwenye ujauzito wa wiki 11( miezi miwili na wiki moja) alisema kwa
muda mrefu mtuhumiwa huto Badri Juma alikuwa akimtongoza ambapo
alimfuata nyumbani kwao majira ya saa 6 usiku baada ya wazazi wake
kwenda msibani na kumwacha na wadogo zake na kumshawishi kuondoka naye
hadi kwake.
Alisema
walipofika nyumbani hapo mtuhumiwa huyo alimvua nguo kisha akampatia
sh. 20,000 na kumwingilia,hata hivyo baada ya kutimiza haja zake
alimnyang’anya fedha hizo na kumrejesha tena kwao usiku huo huku akimpa
ahadi ya kumpa matumizi na nguo lakini hakutimiza ahadi hiyo.
Afisa
Elimu Msingi Wilaya ya Magu, Glory Vicent Mtui alisema alimpongeza mkuu
wa wilaya hiyo kwa jinsi anavyoshughulikia changamoto ya mimba
kuhakikisha wahusika wanakamtwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
na kuahidi hawatafumbia macho suala la mwanafunzi huyo licha ya baadhi
ya wazazi kuwaficha wahalifu kwa kupewa rushwa sababu ya mazingira
magumu na umasikini.
Tangu
Januari mwaka huu takwimu za mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi ni
28 na siamini mzazi yeyote anafurahia mwanaye kukatishwa masomo na hili
tatizo l mimba tutafanya kazi ya kukabiliana nalo na kuhakikisha
wahusika wanakamatwa na kufikishwa mahakamani na hadi sasa zipo kesi 28
baadhi ziko mahakamani na zingine watuhumiwa wamekimbia ama kuachiwa
sababu ya changamoto ya rushwa kwa mashahidi, ”alisema Mtui.
Aidha,
Afisa Mtendaji wa Kata Kahangara, John Clavery Mabati, alisema kuwa
mtuhumiwa alipokamatwa na kuhojiwa alikiri kufanya ngono na kumpa
ujauzito mwanafunzi huyo na ili kujinasua na mkono wa sheria alijaribu
kumshawishi kwa kumpa rushwa ya sh.milioni 2 akaikataa.
Alidai
kabla watu waliotumwa kumkamata mtuhumiwa huyo walihongwa kabla ya
kumkamata Novemba 4, mwaka huu ambapo alimfahamisha DC (Mkuu wa Wilaya)
naye akaagiza asiachiwe ndipo wakamfikisha polisi kwa hatua za kisheria.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Ijinga, Ncheyeki Casmir alisema mwanafunzi huyo
ambaye alikuwa miongoni mwa 10 waliopelekwa kwenye vipimo vya
mimba,alibainika kuwa na ujauzito na hakuwahi kuwaeleza wazazi kitendo
alichofanyiwa.
Alisema
walipomhoji mwanafunzi huyo aliwaeleza kila kitu kuhusu suala hilo na
kwamba siku wazazi wake wakiwa wamekwenda kulala msibani usiku mtuhumiwa
alifika nyumbani kwao akamshawishi wakaondoka naye usiku huo kwenda
naye nyumbani kwake ambako alimwingilia huku akimhaihidi kumhudumia.
Naye
Mama mzazi (jina linahifadhiwa)wa mwanafunzi huyo alisema licha ya kuwa
wanalala nyumba moja na binti yake hakuwahi kumweleza lolote kuhusu
Badri na alipata taarifa ya ujauzito kutoka kwa walimu baada ya kuitwa
shuleni na kuelelezuwa binti yake ana ujauzito wa wiki 11.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Ijinga Kisiwani, Ncheyeki Casmir (mwenye shati
ya drafti) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa hbari kuhusu utaratibu
unaotumika shuleni hapo kubaini wanafunzi wenye ujauzito.
Afisa
Elimu Msingi Wilaya ya Magu, Glory Mtui akitoa takwimu za wanafunzi
walioapata ujauzito wilayani humo kwa mwaka huu ambapo tangu Januari
watoto 28 wamebainika kuwa na mimba. Picha zote na Baltazar Mashaka
Mama
wa mtoto aliyepewa ujauzito (jina linahifadhiwa) na mwenyekiti wa
kijiji akieleza jinsi alivyopokea taarifa za ujauzito aliopata mwanaye.
No comments:
Post a Comment