TAWLA:FUTENI KANUNI ZILIZOWEKWA NA TUME YA UCHAGUZU KUEPUKA KUCHOCHEA VURUGU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 22, 2020

TAWLA:FUTENI KANUNI ZILIZOWEKWA NA TUME YA UCHAGUZU KUEPUKA KUCHOCHEA VURUGU

 

 

Baadhi ya Washiriki wa kikao Cha wadau wa uchaguzi mkoa wa Arusha wakifuatilia mjadala ulikuwa ukiendelea,mbele yao ni Frimin Miku mwezeshaji katika kikao hicho
Kaimu Shekhe mkoa wa Arusha akichangia mada katika kikao Cha wadau wa uchaguzi mkoa wa Arusha kilichoandaliwa na TAWLA
Baadhi ya Washiriki wa kikao Cha wadau wa uchaguzi mkoa wa Arusha wakifuatilia mjadala    ulikuwa ukiendelea,mbele yao ni Frimin Miku mwezeshaji katika kikao hicho
Wa kwanza Kushoto ndugu  Mabula kutoka katika ofisi ya       Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa na baadhi ya Washiriki wa kikao Cha wadau wa uchaguzi mkoa wa Arusha wakifuatilia mjadala ulikuwa ukiendelea,mbele yao ni Frimin Miku mwezeshaji katika kikao hicho
Baadhi ya Washiriki wa kikao Cha wadau wa uchaguzi mkoa wa Arusha wakifuatilia mjadala ulikuwa ukiendelea,mbele yao ni Frimin Miku mwezeshaji katika kikao hichoNa.Vero Ignatus,Arusha

Watanzania wametakiwa kuhakikisha wanafuata kanuni taratibu zilizowekwa na tume ya Uchaguzi kwa lengo kutochochea vurugu wakati wote wa zoezi la upigaji wa kura.

Aidha tume ya Uchaguzi iwe muangalizi wa misingi ya Demokrasia wakati wote wa uchaguzi Ili kuendana na Uchaguzi huru na haki.

Hayo yamesemwa na Chama Cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) katika kikao Cha wadau wa uchaguzi kutoka Asasi za Serikali na zile za Kiraia mkoa wa Arusha kwa lengo la kujadili uendeshaji wa uchaguzi na wajibu wa kila mdau.

Mratibu wa TAWLA mkoa wa Arusha Happyness Mfinanga , alisema kuwa Dira ni kuhamasisha jamii ,kulinda na,kutetea wanawake kwa kutoa Elimu juu ya ubaguzi wa Kijinsia ,ambapo katika upigaji kura kwaajili ya kuchagua Viongozi na wanakwake pia wapo hivyo lazima waheshimiwe.

Mfinanga alisema kuwa dhumuni lao ni kuendelea wanawake Kama vinara katika kutetea, kulinda haki za wanawake ,na utawala bora kupitia Elimu ya kisheria huku alisema itikafi yao ni uwajibikaji, uadilifu,utofauti,kujitolea na utaalam.

Akizungumza mwezeshaji wa mjadala huo Firmin Miku aliwaongoza wadau hao,katika   kuangalia  ya Uchaguzi,siku ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi jinsi ya kuweza kufanya Uchaguzi wa kidemokrasia 

Sambamba na hayo Waliweza kujadili kwa kina juu ya wajibu wa kila mdau, katika Uchaguzi mkuu Ikiwemo Tume ya Uchaguzi, kwani ndiyo yenye jukumu la kutangaza matokeo ya Uchaguzi haswa ya Urais.

Aidha katika ngazi za majimbo wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi kuratibu upatikanaji wa rasilimali fedha, kwaajili ya kukamilisha na kusimama taratibu zote za Uchaguzi ,sambamba na  kuhakikisha Uchaguzi kunakwenda Kama ulivyopangwa.

Akichangia mada katika kikao hicho kutoka Taasisi ya Women and Children Vision (WOCHIVI) Faith Swai ,alisema ufike wakati vyombo vya Ulinzi na Usalama vipatiwe Elimu, juu ya Jinsia Ili hata wanapomkamata mtuhumiwa mwanamke, watambue namna ya kukumfikisha eneo husika bila kumdhalilisha 

"Wakati mwingine ukiwaona baadhi ya Askari wanavyowakamata watuhumiwa mwanamke, ukweli inaumiza hivyo tunawaomba wahusika mtusaidie kutoa Elimu juu ya Jambo hilo "Alisema Faith

Swai aliweza kuongeza kwa kusema kuwa ufike wakati vyama vya siasa ,vitoe elimu juu ya matumizi ya lugha njema wawapo majukwaa ya siasa ,bila kuwadhalilisha wanawake, katika Kampeni zao.

 Chama Cha Wanasheria nchini Tanzania  (TAWLA) kiliwataka wadau hao, Kutambua kuwa kupiga kura kwa mwananchi aliyekidhi vigezo, ni haki yake ya Msingi hivyo ifikapo tarehe 28/10/2020 ni vyema wakapige kura kwaajili ya kumchagua viongozi wanaomtaka, kwajili ya maendeleo ya Taifa lao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad