MAJAJI NA MAHAKIMU WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI VISIWANI PEMBA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 19, 2020

MAJAJI NA MAHAKIMU WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI VISIWANI PEMBA

 

 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu akiwa katika pivha ya pamoja na majaji ya mahakimu  wa Zanzibar.

Jaji Mstaafu Januari Msofe akitoa mada kwenye semina ya majaji na mahakimu kisiwani Pemba ikiwa ni maandalizi ya kukabiliana na kesi za uchgauzi

………………………………………………………………………………..

Na Masanja Mabula , PEMBA

JAJI Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu amewataka Majaji  na Mahakimu visiwani humo kuzisoma vyema na kuzielewa  sheria na kanuni za uchaguzi ili ikitokezea malalamiko yanayohusu uchaguzi wawaze kuyapatia ufumbuzi kwa haraka kwa kutoa haki kwa mujibu wa sheria.

Akifungua mafunzo ya siku mbili wa Majaji na Mahakimu  yanayofanyika Wesha Kisiwani Pemba Jaji Makungu alisema  kutokana na vuguvugu linaloendelea wameona ni vyema kufanya semina ya kujiandaa kukabiliana na malalamiko yatayowasilshwa baada ya uchaguzi.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018 iliyotungiwa kanuni imetoa maelekezo ya kesi za uchaguzi kukamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

“Sheria ya uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018, ambayo imetungiwa kanuni mwezimseptemba mwaka 2020 zimetoa maelekezo ya kesi za uchaguzi kukamilika ndani ya kipindi cha miezi kumi na mbili”alifahamisha.

Naye Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa John Mroso alisema ni vyema majaji na mahakimu kutenda haki ili mwenye haki apate haki yake.

Alisema ni vyama majaji na mahakimu kuituma elimu watakayopatiwa kuendesha kesi za uchaguzi kwa weledi ili kuepuka malalamiko kwa atakayekosa haki.

“Ni vyema Majaji na Mahakimu kujiandaa kukabiliana na malalamiko ya uchaguzi baada ya matokea kutangazwa ili waweze kutoa haki na mwenye haki”alisisitiza.

 Naye Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Fatma Mahaoud alisema iwapo kesi zitatokea wamejiandaa kukabiliana na nazo.

“Hatupendi kutokea malalamiko baada ya uchaguzi, lakini ikitokea yameripotiwa sisi tupo tayari kuyafanyia kazi kwani ndio kazi yetu”alisema.

Mapema mwakilishi wa shirika UNDP  Salma Ali Hassan alisema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo majaji na mahakimu ni kumaliza kesi kwa muda mfupi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad