HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 22, 2020

DC ARUMERU AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 165 KWA VIKUNDI 37 VYA WANAWAKE,VIJANA NA WALEMAVU

 


 Na Jusline Marco;Arumeru

MKUU wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro mekabidhi hundi ya shilingi millioni 165 kwa vikundi 37  ikiwa ni awamu nyingine ya kwanza ya mikopo iliyoanza kutolewa ambayo inawalenga wanawake, vijana na walemavu.

Akikabidhi hundi hiyo Muro amesema hadi sasa zaidi ya vikundi 550 vya wananchi wilayani humo tayari vimepatiwa mikopo kupitia fedha zinazotokana na asilimia 10 ya Mapato ta ndani ya Halmashauri ambapo jumla ya shilingi bilioni 3 zimeishatolewa katika vikundi mbalimbali vilivyoundwa na makundi hayo ya wananchi Ili kuwakwamua kiuchumi.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano Halmashauri zote mbili za Meru na Arusha vijijjni zimeweza kufikia malengo kwa kuyafikia makundi yote matatu kwa haraka kutokana na mwitikio wa wananchi wa kujitokeza na kuanzisha miradi ambayo imekuwa endelevu hali iliyopelekea kuwa na wanufaika 6000 waliopatiwa mikopo hiyo kuanzia mwaka 2015/2016 mpaka kufika mwezi September 2020/202.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa utoaji wa mikopo isiyokuwa na riba kupitia asilimia 10 ya makusanyo ya fedha za ndani za Halmashauri, mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ta Arusha vijijini Bi. Angelah Mvaa amesema  Halmashauri hiyo inaendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuanzisha na kuwajengea uwezo kupitia program ya mafunzo maalum kwa vikundi wanufaika itakayowasaidia kuweza kuzitumia fedha hizo katika njia iliyokusudiwa.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi hiyo baadhi ya wanawake na vijana mbali na kumpongeza, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika kusimamia alichoahidi katika ilani ya Uchaguzi katika kipindi cha mwaka 2015/2020 wamesema kasi ya serikali ya awamu ya tano katika kuwafikia na kuyabadilisha maisha yao imefanikiwa kwa kiasi likubwa.

Aidha serikali imeendelea kuwajali na wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha hawaachwi nyuma kwenye uchumi wa kati ambapo mmoja kati ya wanufaika wa mikopo hiyo, Bi.Suzan Eliamsuri kutoka kata ya Mateves, amesema mikopo hiyo imekuwa mkombozi wao.

Hata hivyo hafla ya makabidhiano ya fedha hizo imekwenda sambamba na utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali kwa akina mama, vijana na watu wenye ulemavu sambamba na uanzishwaji wa vikundi vingine ambavyo vitaendelea kujengewa uwezo kabla ya kukabidhi fedha zingine katika awamu ijayo.


 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad