WANAWAKE NGORONGORO KUNUFAIKA NA ZAO LA NGOZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 6 September 2020

WANAWAKE NGORONGORO KUNUFAIKA NA ZAO LA NGOZI

 


Baadhi ya wakinamama kutoka jamii ya Kimasai walionufaika na mradi wa Gift Fund kutoka Oxfam ambao uliowafikia kwa kupitia Palisep.
Nolamala Nndeenye kutoka Engisorisambu Kijiji cha Orkiu B mmoja ni mmoja wa wanufaika wa mradi huo wa Gift fund kutoka Oxfam iliyowafikia kwa kupitia Palisep

Baadhi ya wakinamama wlaionufaika na mradi wa Gift fund kutoka Oxfam

Mkurugenzi mtendaji wa Palisep Robert Kamakia akiwa na wakinamama jamii ya Kimasai kwenye jengo walilopewa na halmashauri ya (w)ya Ngorongoro kwaajili ya kutekeleza shughuli zao za kiujasiriyamali

Bi Noorkishire Kiriku kutoka kata ya Nguserusambu ambae ni katibu wa kikundi akifurahia moja ya mashine ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngozi.
Wakinamama kutoka jamii ya Kimasai wakifurahia moja ya mashine ambayo wataitimia kurahisisha kazi za uzalishaji wa bidhaa za ngozi.

Noorkiyengop Mbaima kutoka kata ya Engisorisambu kijiji cha Erkiu:mradi huo kwake una faida kubwa kwani umemsaidi sio kujikwamua kiuchumi tu pia amepata mafunzo ya kujitambua hata akathu utu kuchukua hatua ya kugombea uongozi Jambo ambalo kwake amesema ni hatua kubwa.
Afisa mifugo wa wilaya ya Ngorongoro Kaayenye Samson Laizer akitoa ufafanuzi juu ya zao la ngozi na namna ilivyo ya thamani ikiwa haijawekwa alama.


Mkurugenzi mtendaji akibadikishana mawazo na mkaguzi wa mradi huo kutoka Oxfam Dastan Kamanzi.Na Vero Ignatus

Shirika la Oxfam limetoa masaada wa Gift Fund kwa wananchi katika Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,katika kuwaongezea uwezo wa kuzalisha bidhaa za ngozi ,ufugaji bora ,pamoja na kuwapatia mafunzo ili waweze kuzalisha bidhaa mbalimbali zitokanazo na zao la ngozi kwa kutumia mashine walizonunuliwa

Robert Kamakia ni Mkurugenzi mtendaji wa Palisep anasema kuwa mara baada ya kupokea msaada huo, kwa upande wao waliangalia masuala ya usawa wa kijinsia katika jamii ya kifugaji pamoja na namna ya kujikwamua kiuchumi,hivyo walielekeza mradi huo kwa wanawake na vijana kwaajili ya kuzalisha bidhaa za ngozi

Robert anasema wameamua kuelekeza mradi huo kwa wanawake, kwani changamoto kubwa katika jamii ya kifugaji ,ni pale ambapo mwanamke anapokuwa na uwezo na kujaribu kwenda kwenye ngazi ya familia,na kuonekana anatakiwa ashirikishwe kutoa maamuzi kwenye katika familia,anaonekana mwanamke huyo amepotoka na siyo mke yule aliyezoweleka katika jamii ya kimasai

''Wanawake wengi wamekuwa wakiwasihi waume zao kwamba kabla hatujauza ng'ombe tuongee katika familia,hata masaini mifugo yote ni ya baba,hivyo mwanaume anaweza kuuza na akaenda kunywa pombe na mwanamke haruhusiwi kuuliza,sasa kwa uwezo tulioujenga ni kwamba wanawake wanaouwezo wa kuwaambia waume zao tujadiliane katika ngazi ya familia ndipo tuchukue maamuzi ''Anasema Robert.

Robert anasema kuwa 90% ya wakazi wa Ngorongoro ni wafugaji hivyo walifanikiwa kuunda kundi la watu 30,ambao waliwagawanya katika idadi ya watu 10 , kila kundi linajukumu la kufanya ikiwepo kutafuta masoko,uzalishaji wa bidhaa pamoja na uongozi, anasema mradi huo wa Gift walioupokea kutoka Oxfam unatekelezwa katika vijiji vitatu ikiwemo Waso,Sale na Orkiu juu.

Aidha changamoto kubwa waliyokutana nayo katika utekelezaji wa mradi huo ni pamoja na kuzuka kwa ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona 19, ambayo iliwalazimu kila mmoja wao kubakia nyumbani kwake, na kushinda kukutana,pamoja na changamoto ya kisiasa

kwa upande wake Afisa mifugo wa wilaya ya Ngorongoro Kaayenye Samson Laizer anasema Serikali ilianzisha mkakati wa kuboresha zao la ngozi mwaka 2007 -2008 na ikawekwa sheria namba 18 ya mwaka 2008 juu ya kuboresha zao hilo kwa halmashauri 55 na baadae wakaongeza halmashauri 10 jumla zifikia 65

Laizer anasema katika kutekeleza sheria hiyo, serikali ilitafuta wafadhili mbalimbali ,(huku akikiri kuwapokea Palisep ambao wanatekeleza mradi kutoka Oxfam) ambao watasaidia kutekeleza mkakati huo katika mazingira ya kutengeneza ajira kwa wajasiriyamali katika eneo la ufugaji , ambapo jamii ilitakiwa kwanza ipate elimu ya kutosha juu ya ushindani wa soko la bidhaa husika

''Mwanzoni wafugaji wa kimasai walikuwa hawaijali ngozi kabisa, walichokua wanajali wao ni ile brand kwamba kila mtu anakuwa na alama yake,kila mtu anamchorachora mnyama wake vile apendavyo,hawakujua kwamba ngozi ya mifungo ina impact kubwa na ina bei,sasa baada ya kuwa na ile sheria tukajaribu kuwapa watu elimu kwamba ngozi ni kitu cha thamani sana ''Anasema Laizer

Aidha katika zao la ngozi yapo madaraja tofauti ikiwemo la 1-3 pamoja na ngozi chakavu,hivyo wamechukua jukumu la kuwaelimisha wafugaji ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo ya machinjio,kwamba watambue thamani,pia wajue kuwa ngozi ndizo zinatumia katika kutengenezea bidhaa mbalimbali,pia wameweza kuwasaidia wafugaji kuelewa kuwa ngozi isipokuwa na alama uwa bei yake ni nzuri tofauti na ile yenye alama

Akizungumza mnufaika wa mradi huo Noorkiyengop Mbaima kutoka kata ya Engisorisambu kijiji cha Erkiu juu ameshukuru kwa mradi huo kwani umefika katika jamii haswa kwa wanawake,amesema wameweza kupata mafunzo mara 3 kutoka Palisep ambayo yatawasaidia wao wenyewe na jamii nzima namna ya kujikwamua kiuchumi.

Mbaima anasema wakifanya kazi hiyo ya zao la ngozi watapata fedha,kwani mafunzo waliyoyapata ni endelevu na wamepata vifaa vya kutendea kazi kwani hapo awali walikuwa wakitumia mikono na kupoteza muda mwingi,ila sasa watazalisa kwa wingi zaidi na faida kubwa itaonekana.

Kwa upande wake mnufaika mwingine wa mradi huo wa Gift Nolamala Ndeenye kutoka Engisorisambu Kijiji cha Orkiu B :mafunzo hayo yamewasaidi wao kujua namna ya kuandaa na kutengeneza ngozi,ambapo yeye ameahidi kwamba ataisaidia jamii yake pamoja na kuhakikisha kuwa watoto wake wanapata elimu bora

Ameomba Oxfam na Palisep wawatembelee mara kwa mara ili kuwajengea uwezo zaidi na kuona uzalishaji wao unavyoendelea,kwani mara zote mwanzo wa jambo huwa ni mgumu ila wakipata uwangalizi mzuri watapata manufaa zaidi.

Bi Noorkishire Kiriku kutoka kata ya Nguserusambu ambae ni katibu wa kikundi anasema mafunzo hayo kwake yanafaida kubwa kwake kwani zamani alikuwa hafahamu thamani ya ngozi,ila baada ya mafunzo ameelewa vyema,anasema wamefundishwa hata namna ya kuchinja ng'ombe,mbuzi,ambapo kipato cha awali wanatazamia kupata tsh 500,000 na baadae wataendeleza zaidi

Amesema kwa sasa wameshajifunza namna ya kutumia mashine hizo, hivyo wanatarajia kuanza kazi rasmi baada ya changamoto ya corona kupungua,anasema mwanzoni wao kama wanawake katika jamii ya wamasai walikuwa hawaruhusiwi kumiliki ng'ombe ,ila kwa sasa baada ya mafunzo kila mama ana ng'ombe anayemfuga kwaajili ya kujipatia kipato kwa zao la ngozi .

Kwa mujibu wa sensa ya idadi ya watu iliyofanyika mwaka 2012 idadi ya watu halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ni 174,278,vitongoji 253,wastani kukua kwa kaya 4.5% idadi ya ng'ombe takribani 483,387,idadi ya shule za sekondari 10,shule za msingi 67,idadi ya tarafa 3 na idadi ya kata ni 28.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad