MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa
Kata ya Mzizima Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akimnadi mgombea
udiwani wa Kata ya Mzizima Fredrick Chiluba wakati wa mkutano wake wa
kampeni
Mgombea
udiwani wa Kata ya Mzizima Fredrick Chiluba kushoto akimuombea kura
mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia wakati wa
mkutano wake wa kampeni
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na mgombea
udiwani wa kata ya Mzizima Fredrick Chiluba wakifuatilia matukio
mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba
Msanii Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema akichaguliwa kuwa
mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha anajitahidi kuanzisha ujenzi wa
hosteli kwa wanafunzi wanaosoma shule za sekondari wanaokaa mbali ili
kuwawezesha kusoma bila uwepo wa vikwazo.
Hatua
hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule za Sekondari
kukaa mbali na maeneo ya shule hali inayopelekea kushindwa kufika kwa
wakati kutokana na changamoto ya usafiri.
Ummy
aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mzizima katika
uwanja wa Gogovivu kwenye mkutano wake wa kampeni ambapo alisema suala
hilo litakuwa mwarobaini wa kuwaepusha wanafunzi kutokufika shuleni.
“Ninaamini
ujenzi wa Hostel utasaidia kupunguza changamoto ambazo zinawakabili
wanafunzi wanaosoma shule za mbali kutokana na kukosekana kwa usafiri
kwa baadhi ya maeneo wanayokwenda”Alisema
Hata
hivyo alisema kwamba ataendelea pia kushirikiana nao kujenga
miundombinu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi
na sekondari.“Ninafahamu shule za msingi Mafuriko,amboni,rubawa na
mleni kuna maadhibi miomdnboni sio mizuri na madarasa
hayatoshi,ninawaomba sana ..mchango wangu niliiutoa kabla sijawa mbunge
niaminini niweze kushirikiana nanyi kuboresha elimu hasa miundombinu na
kutafuta madawati kwa ajili ya wanafunzi”Alisema Ummy
“Lakini
pia sijaisahau shule ya sekondari Kiomoni nimewekeza ujenzi wa madarasa
mawili ninawaomba sana mnichague ili tuweze kuiboresha zaidi”Alisema
Hata
hivyo alisema pia atalazimika kubadilisha jina la shule ya sekondari
Kiomoni kwa sababu ni ya shule ya kata ya Mzizima hivyo watabadilisha
jina liweze kuwa shule ya sekondari Mzizima.
“Niaminini
tuweze kutatua changamoto za wanafunzi wa Rubawa,Mleni ambao wanakwenda
mpaka sekondari ya kiomoni kwa usafiri wenye changamoto na kupelekea
kushindwa kufika shuleni kwa wakati”Alisema
No comments:
Post a Comment