Dr.
Steve Meyer akiwa na Dr bingwa wa mifupa kutoka hospitali ya Mount Meru
Dr Elias Mashalla na mjumbe wabodi ya stemm na mgombea ubunge jimbo la
Arumeru magharibi kwenye kontena lenye vifaa vya mifupa liko katika
kituo cha watoto yatima Cha stemm,Mbuguni
Wa
kwanza kushoto ni mke wa Dr Steve Meyer,wa pili Dr Steve Meyer
,akifuatiwa na mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Dr focus Maneno.
Na.Vero Ignatus.
Shirika
lisilo la Kiserikali la Stemm linalojishughukisha na Elimu,Afya na
watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi limekabidhi
vifaa vya upasuaji wa mifupa na afya vyenye thamani ya shilingi bilioni
4.5 kwa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Arumeru, mkoani Arusha.
Akikabidhi
msaada huo Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo DR,STEVEN MEYER katika kituo
cha watoto yatima kilichopo kijiji cha Kikuletwa , kata ya mbuguni
,wilaya Arumeru, amesema lengo la msaada wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya
wanafunzi watatu walionusurika katika ajali iliyohusisha gari la shule
ya msingi Luck vincent iliyotokea mwezi meii mwaka 2017, na kusababisha
vifo vya wanafunzi 32, waalimu 2 na dereva 1 eneo la Rotia wilaya ya
Karatu.
Hata
hivyo amesema kuwa vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa hospitali za
mkoa wa Arusha pindi wagonjwa watakapohitaji matibabu ya mifupa; huku
akimshukuru Rais Dr,John Magufuli kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya
afya hasa kufanikisha upatikanaji wa hati za kusafiria manusura
wanafunzi wa ajali hiyo ambao ni Doreen ,Elibariki,Sadia Awadh na Wilson
Godfrey ambapo kwa sasa wanasoma kidato cha tatu katika shule ya
sekondari ya Star High School .
Akipokea
msaada huo Mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Dr, Focus Maneno alimesema
kuwa umekuja wakati muafaka ambapo hospitali hizo zinahitaji vifaa hivyo
kwa matibabu ya wagonjwa wa mifupa.
Amesema
kuwa licha ya msaada huo bado wanakabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa
wa mifupa ambapo inawalazimu kuwapa rufaa kwenda kwenye hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Arusha
Kwa
upande wake mjumbe wa bodi ya Stemm ambae pia ni mgombea Ubunge wa
jimbo la Arumeru Mashariki Dr.John Palangyo kwa niaba ya wanachi wilaya
ya Arumeru ameshukuru kwa vifaa hivyo ambavyo vitakuwa msaada mkubwa
hasa kipindi hiki ambapo watanzania wanahitaji zaidi huduma za afya ya
mifupa na kupunguza gharama za kutibiwa nje ya nchi.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Kikuletwa Hosea Palangyo amelishukuru Shirika hilo kwa
kuwapatia vifaa hivyo kwani wananchi walikuwa wanatumia gharama kubwa
kufuata matibabu ya mifupa nje ya Wilaya hiyo,sambama na kutoa fedha
kiasi cha shilingi laki nne kwa mwezi kusaidia chakula kwa shule
zilizoko katika kata ya mbuguni.
No comments:
Post a Comment