HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 29, 2020

LATRA YATANGAZA NAULI MPYA ZA TRENI YA ABIRIA MOSHI- ARUSHA

 

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli za treni ya abiria itakayofanya safari zake kutoka Moshi mjini hadi Arusha na kurudi Moshi.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Arusha leo tarehe 29 Septemba, 2020, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe amesema nauli hizo zimetangazwa kufuatia Shirika la Reli Nchini (TRC) kuwasilisha maombi ya nauli hizo, ambapo LATRA ilifanya mikutano ya kupokea maoni ya wadau, kisha kufanya uchambuzi wa maoni hayo pamoja na kuchambua mchanganuo uliowasilishwa na TRC. 


Kwa mujibu wa kifungu cha 21 (2) (b) cha Sheria ya LATRA namba 3 ya 2019, baada ya mchakato wa uchambuzi kukamilika, Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA imeidhinisha nauli hizo na kuainisha nauli zitakazotumika kwa usafiri wa treni ndani ya mikoa hiyo na nje ya mikoa kama inavyoonekana katika jedwali.


Nauli zilizoidhinishwa na LATRA zikionesha mchanganuo wa vituo vya ndani nan je ya mikoa husika



KUTOKA MOSHI KWENDAUmbali (KM)NAULI KWA MADARAJA HUSIKA (SHS):
Daraja la tatuPili kukaa
1RUNDUGAI221,0001,500
2KIKULETWA311,0001,500
3KIA371,0001,500
4USA RIVER621,5002,000
5TENGERU651,5002,000
6CHEKERENI751,5002,000
7NJIRO821,5002,000
8ARUSHA861,5002,000

KUTOKA ARUSHA KWENDAUmbali (KM)NAULI KWA MADARAJA HUSIKA (SHS):
Daraja la tatuPili kukaa
1NJIRO41,0001,500
2CHEKERENI111,0001,500
3TENGERU211,0001,500
4USA RIVER241,0001,500
5KIA491,5002,000
6KIKULETWA551,5002,000
7RUNDUGAI641,5002,000
8MOSHI861,5002,000


Nauli za wanafunzi kutoka mwanzo hadi mwisho wa safari ni Sh. 300.00 kwa daraja la tatu, na Sh 400.00 kwa daraja la pili kukaa.

Mkurugenzi Mkuu LATRA Gilliard Ngewe akimkabidhi Henry Machoke, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara TRC andiko la nauli zilizoidhinishwa

Wakati huo huo, LATRA imeiagiza TRC kutekeleza masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya usalama kwa wadau husika, kutumia mfumo wa tiketi za kielektroniki, kutoa ratiba za safari kwa umma, kutekeleza hatua za usalama kudhibiti msongamano wa abiria, kuboresha miundombinu na huduma za kijamii, kuweka kitengo cha huduma kwa wateja na kutangaza nauli zilizoidhinishwa katika vyombo mbalimbali vya habari ili ziwafikie wadau wengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad