HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 29, 2020

AKINA MAMA NI JESHI KUBWA TUKIWAPA NAFASI WANAWEZA

 

 Na Abdullatif Yunus MichuzTv.


Katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinaibuka na Ushindi wa Kishindo kwa Wagombea wake nafasi zote, Mikutano ya Kampeini imeendelea maeneo mbalimbali hapa Nchinj, lengo likiwa ni Kunadi sera na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na Wagombea wake.


Akiwa katika Majimbo ya Uchaguzi ya Bukoba Mjini na Bukoba Vijijini, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Mkoa Kagera Ndg. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa Nyakati tofauti amefanya Mikutano miwili ya Kampeini Septemba 28, 2020 na kuwanadi Wabunge Wateule wa majimbo hayo Dkt. Jasson Samson Rweikiza (Bukoba Vijijini) Wakili Stephen Byabato (Bukoba Mjini) pamoja na Madiwani wa CCM wa Majimbo hayo.


Katika kuwapa msisitizo wapiga Kura wachague kilicho Bora Ndg. Majaliwa amewaomba kufanya maamuzi sahihi ya ya kuchagua Chama Cha Mapinduzi na kwamba endapo watafanya hivyo watakuwa na bahati ya kuwapata Wabunge Wanne zaidi katika zile nafasi za Viti maalum, na kwamba Ni bahati ya pekee kwa Mkoa wa Kagera kuwa na Uwakilishi Mkubwa wa namna hiyo hivyo maendeleo hayatakwama.


Kwa Upande wake Regina Samuel Zachwa Mbunge Mteule Viti Maalum UWT Kagera wakati wa kuomba Kura amewaomba Wananchi kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwakuwa ndicho Chama pekee kinacholeta maendeleo, licha ya Maendeleo hayo yamekuwa yakitumiwa pia na wasiokuwa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, huku akikumbusha Juu ya Umuhimu wa akina mama katika Jamii, kuwa Wanawake ni Jeshi kubwa ambalo kimsingi wakiaminiwa wanafanya makubwa, hivyo endapo watakipa ridhaa Chama Cha Mapinduzi watakuwa wamewapa nafasi ya kuwatumikia Kama wawakilishi wao.


Mikutano Kama hiyo inaendelea Tena Septemba 29, 2020 katika Majimbo ya Uchaguzi ya Kyerwa, Karagwe na Missenyi.

 Ndg. Kassim Majaliwa Viwanja Mlezi wa Mkoa Kagera akimsikilza kwa umakini, Mbunge Mteule Viti Maalum UWT Regina Zachwa wakati akipitia mipango iliyoanishwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Mkoa wa Kagera 2020 Hadi 2025.

 Mbunge Mteule kutoka Taasisi na Asasi za Kiraia NGOs Neema Lugangira akifafanua vyema kuhusu umuhimu wa kukipigia Kura Chama Cha Mapinduzi wakati akiomba Kura Jimbo la BukobaVijijini

 Mbunge Mteule UWT Kagera Bernadetha Kasabago Mshashu anaonekana akiomba Kura kwa Wananchi wakati alipopewa nafasi ya Kufanya hivyo

 Kwa unyenyekevu Mkubwa Mbunge Mteule UWT Kagera Regina Zachwa akipiga magoti kuomba Kura za Rais Magufuli, Mbunge Rweikiza na Madiwani wa CCm katika Mkutano wa Kampeini BukobaVijijini.

Mapema Uwanja wa Ndege wa Bukoba Viongozi wa CCM Mkoa Kagera wakiwa wamejipanga kumpokea Mlezi wao Ndg. Kassim Majaliwa Majaliwa Septemba 28 Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad