HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 5, 2020

WANANCHI WA MKOA WA SIMIYU WATEMBELEA MABANDA TAASISI ZA SEKTA YA UCHUKUZI MKOANI SIMIYU



Afisa Uhusiano wa Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), Bi. Amina Uddi, akimwelekeza mwananchi namna ya kuvaa boya, wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Bi. Ruth Kigera, akigawa kipeperushi kwa mwananchi wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya VIwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mariam lusewa, akiwaonesha wananchi viwanja ambavyo vinatumika kusafirishia mazao, wakati wananchi hao walipotembelea banda la mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mwananchi ambaye hakutaja jina lake, akifafanua jambo kwa Meneja wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Mkoani Mwanza, Bw. Hamid Mwikombe (aliyekaa), wakati wa maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu. Kushoto ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Asha Mwikombe.
Mkufunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Bw. Azan Juma, akiwaonesha sehemu ya kuwekea upepo boya, wanafunzi wa sekondari wakati walipotembelea banda la chuo hicho katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mtaalam wa Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Bi. Mecklina Merchades, akiwaeleza wakazi wa Simiyu namna wanavyosoma viwango vya joto wakati wa usomaji wa hali ya hewa, wakati wakazi hao walipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Afisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Julius Alute, akitoa maelezo ya bandari zinazomilikwa na Mamlaka hiyo wakati wakazi hao walipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Salum Pazi akitoa maelezo kwa wanafunzi wa sekondari kuhusu shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo, wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Bi. Regina Tarimo akitoa maelezo kwa Watoto waliotembelea banda hilo kuhusu mamlaka treni zinazosafirisha mazao, wakati Watoto hao walipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Kaimu Meneja Biashara na Masoko, Kampuni ya Usimamizi na Uendelezaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA, Azizi Jarufu akitoa maelezo ya aina ya mazao yanayosafirishwa kupitia kiwanja hicho kwa mwananchi, wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonesho ya Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WIzara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad