TAASISI YA YST YATOA TUZO KWA SHULE YA WANAFUNZI WA SEKONDARI YA WASICHANA NGANZA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 9, 2020

TAASISI YA YST YATOA TUZO KWA SHULE YA WANAFUNZI WA SEKONDARI YA WASICHANA NGANZA

Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Young Scientists(YST) imewatangaza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ngaza ya jijini Mwanza Glory Kirochi na Martha Machumu kuwa washindi wa  tuzo ya wanasayansi chipukizi ambayo hutolewa na taasisi hiyo.

YST imesema wanafunzi hao wameibuka washindi baada ya kubuni mradi wa namna ya kuzalisha chakula cha mifugo katika kipindi cha ukame (hydroponic fodder).

Akizungumza katika utoaji wa Tuzo hizo uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, Mwanzilishi mwenza wa YST, Dk Gozberth Kamugisha amesema washindi hao wamepata kikombe, ngao, medali na fedha Sh.1,350,000.

Mbali ya zawadi hizo pia wamepata ufadhili wa masomo yao ya elimu ya chuo kikuu kwa kulipiwa gharama zote na Taasisi ya Karimjee Jivanjee.

Amesema nafasi ya pili ilichukuliwa na wanafunzi kutoka mkoani   Arusha katika  Shule ya Kisimili  ambao ni Albert Mhagama na Stella Kasalla ambao walipata kikombe, ngao, medali na Sh.900,000.

Pia amesema tuzo ya kumbukumbu ya Hatim Karimjee  ilichukuliwa na Rugambwa Sekondari iliyopo mkoani Kagera ambapo wanafunzi Ivony Rio na Dorris Kilonzo waliokuwa na mradi wa kuboresha usalama wa ndani ya gari ambapo wamepata Sh milioni moja, ngao na medali .    

Aidha amesema Lameck Obeid na Dennis Ndahaje wa Shule ya Sekondari ya Katubuka iliyopo Kigoma walipata ufadhili wa masomo baada ya kuja na mradi wao waliouita ‘siri kwa nini wanafunzi wanaotoka familia duni wanashindwa kufikia malengo ya elimu’.

“Hii ilitufanya tubadilishe mifumo yetu na kutumia njia za kidigitali kuwafikia wanafunzi na majiji kukagua kazi hizo na kufanya maamuzi kupitia mtandao,” amesema Kamugisha.

Ameongeza kwamba na maonesho hayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuongeza chachu kwa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi lakini mwaka huu kutokana na changamoto ya Covid-19 yameshindwa kufanyika zaidi ya kutoa tuzo hizo kwa njia ua mtandao.

Hata hivyo amesema wakiwa wanasherekea kufikisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, wana mengi ya kujivunia kwa kuzifikia shule nyingi zaidi na kuleta mabadiliko makubwa katika nyanja ya sayansi na teknolojia.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee ambao ndio wadhamini wakuu, wa maonesho hayo Yusufu Karimjee amefafanu kwamba mpaka mwaka jana jumla ya wanafunzi 29 waliofanya vizuri katika YST wanafadhiliwa masomo yao ya elimu ya juu.

Mwisho
[21:58, 03/08/2020] Saidi Mwishehe Michuzi: RITA IMEZUNGUNMZIA UMUHIMU WA KUASILI WATOTO KISHERIA ILI KUWEZESHA KUPATA MAHITAJI YAO YA MSINGI KATIKA JAMII

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umetoa ushauri kwa jamii kuzingatia kusajili cheti /vyeti  vya watoto kisheria pale wanapotaka kuasili mtoto au watoto.

Kwa mujibu wa taarifa ya RITA iliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Agosti 3,2020 imesema inafahamika katika jamii ya kitanzania wapo watoto wanaokulia katika vituo vya kulelea watoto yatima ama kwasababu ya wazazi kufariki, hawajulikani walipo au hawana uwezo wa kuwapatia matunzo.

Vivyo hivyo wapo watu wazima ambao wanashauku ya kuwa na mtoto hata wa kuasili na hiyo ni kwasababu ya pengine kutojaaliwa kuwa na watoto wa kuwazaa.

Imesema Sheria ya mtoto Na.…
[21:59, 03/08/2020] Emm: Asante sana mkuu wangu Mungu wa Mbinguni Akubariki
[21:59, 03/08/2020] Saidi Mwishehe Michuzi: RITA IMEZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUASILI WATOTO KISHERIA ILI KUWEZESHA KUPATA MAHITAJI YAO YA MSINGI KATIKA JAMII

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umetoa ushauri kwa jamii kuzingatia kusajili cheti /vyeti  vya watoto kisheria pale wanapotaka kuasili mtoto au watoto.

Kwa mujibu wa taarifa ya RITA iliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Agosti 3,2020 imesema inafahamika katika jamii ya kitanzania wapo watoto wanaokulia katika vituo vya kulelea watoto yatima ama kwasababu ya wazazi kufariki, hawajulikani walipo au hawana uwezo wa kuwapatia matunzo.

Vivyo hivyo wapo watu wazima ambao wanashauku ya kuwa na mtoto hata wa kuasili na hiyo ni kwasababu ya pengine kutojaaliwa kuwa na watoto wa kuwazaa.

Imesema Sheria ya mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 imeweka utaratibu Kisheria  ili kuweza kusaidia watu wanaotaka kuasili mtoto/watoto kisheria. Kuasili mtoto maana yake ni utaratibu wa kumpatia mtoto aliyekosa mazingira ya kifamilia kupata matunzo ya kudumu ya kifamilia.

"Jumla ya vyeti 863 vimesajiliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kutokana na watu mbalimbali kuleta maombi yao ya kutaka  kusajili cheti cha kuasili mtoto. 

"Ili kuweza kusajili cheti cha kuasili mtoto kisheria katika ofisi za RITA makao makuu muombaji anapaswa kuwasilisha nakala ya uamuzi kutoka  mahakama kuu na pia cheti cha kuzaliwa cha mtoto anayeasiliwa,"imesema RITA kwenye taarifa hiyo.

Imesisitiza ni  muhimu jamii kujua umuhimu wa kusajili cheti cha kuasili mtoto kwani kitasaidia katika kumpatia mahitaji yake ya msingi kama vile elimu,chakula,malazi na masuala ya afya kwa ujumla kama ambavyo watoto wengine wanapata katika jamii. 

"Moja ya haki za mtoto ni kulindwa jambo ambalo watoto wasiokuwa na wazazi wamekuwa wakiteseka kwa kuishi mazingira ambayo si rafiki, mazingira ambayo hayana ulinzi na kupelekea kufanyiwa vitendo viovu na watu wasiokuwa na maadili kama vile kubakwa na kunyanyaswa kijinsia pamoja na mambo mengine.

"Hatahivyo iwapo mtu atasajili cheti cha kuasili sheria itamchukulia kuwa ni sawa na mzazi wa mtoto husika hivyo itasaidia pia kupunguza wimbi la watoto wa mitaani linalokuwa kila kukicha. Hii itasaidia pia kwa Serikali kuweza kupata takwimu sahihi ya wananchi wake katika kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii yake kama vile elimu,"imesema.

Imeongeza kwamba Wakala umetoa ushauri kwa mtu aliyekidhi vigezo vya kuasili mtoto kwa mujibu wa sheria  kuweza kuzingatia kusajili cheti hicho katika Ofiza  za RITA makao makuu Dar Es Salaam  mara baada ya kupata nakala ya uamuzi kutoka mahakama kuu.

RITA inashiriki katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu na huduma zinazotolewa ni Elimu kwa umma kuhusu kuasili watoto, Usajili wa vizazi na vifo, Wosia na mirathi, Ndoa na talaka pamoja na udhamini. Wananchi wanakaribishwa kutembelea banda la RITA namba 94 lililopo upande wa geti la kuingilia karibu na banda la NIDA ili kufaidika na huduma hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad