Nimeshatangaza mgogoro na mameneja NSSF ambao hawafikishi malengo - Waziri Jenista Mhagama - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 4, 2020

Nimeshatangaza mgogoro na mameneja NSSF ambao hawafikishi malengo - Waziri Jenista Mhagama

Nimeshatangaza mgogoro na mameneja NSSF ambao hawafikishi malengo - Waziri Jenista Mhagama

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Ajira,Vijana na Wazee, Jenista Mhagama amefanya ziara katika ofisi za mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mkoani Njombe na kuonyesha kutoridhishwa na utendaji wa kazi ndani ya ofisi hiyo na kutoa agizo kwa meneja wa NSSF mkoa huo kuwa na mkakati mahususi utakaowezesha mfuko huo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa michango.

“Na mimi nimeshatangaza mgogoro na mameneja ambao hawafikishi malengo ambayo sisi tunafikiri wanao uwezo wa kuyafikisha,bodi na mkurugenzi waondoeni hao tutafute meneja mwingine”alisema Jenista

Ni Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Vijana na Wazee, Jenister Mhagama akitoa msistizo kwa Mameneja wanaotumikia ofisi za mifuko ya taifa ya hifadhi ya jamii nchini kuwajibika ipasavyo katika utendaji wao ili kutimiza lengo la serikali wakati alipotembelea ofisi za NSSF mkoa wa Njombe na kuzungumza na wafanyakazi wa mfuko huo na hapa anasema…

“Jambo jingine ambalo nimejifunza hapa hamna mikakati,ipo miradi ya kimkakati ambayo inaendelea kwenye mkoa huu bado hamjaifikia lakini zipo sekta zisizorasmi bado hamjazifikia”aliongeza Jenista

“wote ambao manataka kuwafikia wapo ndani ya wilaya ni lazima mjenge mahusiano vunjeni hizo kuta”alisema Ruth Msafiri mkuu wa wilaya ya Njombe

Awali Meneja wa NSSF mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba akabainisha miongoni mwa changamoto zinazowakabili katika mwaka wa fedha uliopita.

“Uwepo wa wahazini wadaiwa wa michango umepelekea kushindwa kufika lengo la ukusanyanyi pamoja na kuchelewa kulipa wanachama kwa wakati”alisema Mrisho Mwisimba Meneja wa NSSF mkoa wa Njombe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Ajira,Vijana na Wazee, Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watumishi wa NSSF mkoa wa Njombe alipofika mkoani Njombe.
Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akizungumza jambo na Waziri Jenista Mhagama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad