Jaji mstaafu Kaijage amewataka wahariri wa vyombo vya habari kuzingatia maadili ya kazi zao - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 18, 2020

Jaji mstaafu Kaijage amewataka wahariri wa vyombo vya habari kuzingatia maadili ya kazi zao

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Semistocles Kaijage amewataka wahariri wa vyombo vya habari  kuzingatia maadili ya kazi zao, katika kutoa habari kipindi cha kampeni za uchaguzi ili kupunguza joto la kisiasa ambalo linaweza kuhatarisha amani na utulivu,


Wito huo umetolewa leo Agosti 18, 2020 na Jaji Kaijage wakati wa kikao cha Tume hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari kwa lengo la kutoa taarifa juu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu yalipofikiwa hadi sasa.


Amesema tume inatarajia kuona vyombo vya habari vikitoa kipaumbele kwa masuala yanayoelekea kujenga umoja wa kitaifa, badala ya habari ambazo zinaweza kuchochea vurugu kwani kalamu za wanahabari zisipotumika vizuri,zinaweza kuiingiza nchi kwenye machafuko kama ilivyotokea katika maeneo mengine.


"Ninatarajia kuona vyombo vya habari hasa vya umma vinatenda haki sawa kwa vyama vyote kuhakikisha vinatoa  nafasi kwa wagombea wote kujitangaza na kunadi sera na ilani za vyama vyao na kutoa Kipaumbele katika masuala yanayoelekea kujenga umoja wa kitaifa badala ya taarifa na habari ambazo zinachochea vurungu", amesema Jaji Kaijage


Aidha, Tume imevitaka vyama vya siasa na wananchi kuheshimu sheria,katiba na taratibu za uchaguzi kwa kuhakikisha wanazifuata na kuzitelekeleza hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo sheria za nchi na uchaguzi zinaendelea kufanya kazi kama kawaida.


"Sheria za uchaguzi zipo, lakini sheria za nchi pia hazisimamami kwa ajili ya uchaguzi,hakuna kitu kitakachoebda kinyume eti kwa sababu tu kuna uchaguzi, sheria za nchi zipo pale pale", hivyo endapo kutajitokeza matendo ya jina yoyote yatachukuliwa hatua", amesema Jaji Kaijage.


Amesema, baadhi ya wananchi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi watakuwa na joto kali la kisasa wanakuwa hawana utayari wa kuheshimu sheria na taratibu nawaza kufanya kampeni za kistaarabu zisizo ma vurugu na ni vema wote kutambua kuwa sheria za uchaguzi na nchi zinafuatwa.


Ameongeza kuwa, hadi sasa tume imekamilisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kifungu cha 15(5) cha sheria ya taifa ya uchaguzi ambao ulifanyika katika vituo 37,814 vya kuandikisha wapiga kura ambapo jumla ya wapiga kura wapya 7,326,552 waliandikishwa sawa na asilimia 31.63 ya wapiga kura 23,161,440 walioandikishwa Mwaka 2015.


Amesema, kufuatia idadi hiyo ya wapiga kura siku ya uchaguzi kutakuwa na vituo vya wapiga kura 80,155 na kila kituo kimoja kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.

Pia amesema, Tume ya taifa ya uchaguzi imeandaa bajeti kiasi cha shilingi 331,728,258,035.00 ambazo zinatarajiwa kutumika katika uchaguzi Mkuu, fedha ambazo kwa asilimia mia moja zitagaramiwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mfumo Mkuu wa Hazina.


Naye , Mkurungezi wa Tume ya uchaguzi, Dk. Wilson Mahera amesema Tume hiyo inaendelea ma mchakato wa ununuzi wa vifaa na uchapishaji wa nyaraka mbalimbali za uchaguzi na kwamba hadi Sasa zabuni zimeishatagazwa na zinahusisha uchapishaji wa fomu mbalimbali za uchaguzi .


Pia amesema Tume hiyo imejipanga kukutana na wapiga kura ana kwa ana kwa kushiriki katika mikutano mbalimbali ili kuendelea kutoa elimu ya uchaguzi.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage akizungumza na wahariri wakati wa Kikao cha Tume hiyo na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika leo Agosti 18,2020 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JINCC) jijini Dar es Salaam.

 Mkurungezi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dr, Charles Mahera akiongoza majadiliano na kutoa taarifa ya maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020 wakati wa kikao cha Tume hiyo na wahariri wa vyombo mbali mbali jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari na wadau wa Tume ya uchaguzi (Nec) wakifuatilia taarifa ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad