GAVANA LUOGA ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA MAENDELEO TIB NYAKABINDI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 7, 2020

GAVANA LUOGA ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA MAENDELEO TIB NYAKABINDI

Na Mwandishi wetu,
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga ametembelea Banda la Benki ya Maendeleo TIB wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Akiwa bandani hapo alipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
 
Benki ya Maendeleo ya TIB inashiriki maonesho ya Nane Nane ili kutoa elimu kwa umma, kutangaza huduma inayozitoa pamoja na kuvutia wateja wapya kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya kimkakati nchini.
Pia, benki inatumia fursa hiyo kutoa ushuhuda wa miradi ya kimkakati iliyokopeshwa kwa wateja wake waliotapakaa nchini.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga akiongea na wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo TIB wanaoshiriki Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu Benki ya Maendeleo TIB kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Kitaasisi, Bw. Saidi Mkabakuli (kushoto). Wapili kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Bima wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. James Manyama.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo TIB wanaoshiriki Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad