DKT KIMEI AREJESHA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE VUNJO KIMYA KIMYA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 17, 2020

DKT KIMEI AREJESHA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE VUNJO KIMYA KIMYA


Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ,Dkt Charles Kimei akirejesha fomu za kuwania Ubunge Jimbo la Vunjo  ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,anayepokea fomu ni Katibu wa CCM wilaya ya Moshi ,Miriam Kaaya .
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi ,Miriam Kaaya akipitia fomu za Dkt Kimei mara baada ya kuzipokea 
Watia ni wa nafasi za Ubunge katika majimbo ya Moshi vijijini na Vunjo ,Victor na Dkt Charles kimei wakioneshana jambo kwenye simu wakati walipokutana katika ofisi za wilaya ya Moshi kwa ajili ya kuchukua na kurejesha fomu .

Na Dixon Busagaga, Moshi .
JUMLA ya Makada 473 wa chama cha Mapinduzi wamejitokeza
kuwania nafasi ya Ubunge katika majimbo ya mkoa wa Kilimanjaro kupitia kura za maoni huku kati yao 99 ni wale wanaomba nafasi kupitia viti maalumu .

Zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa Fomu za kuwania nafasi
ya Ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi limeendelea huku ikishuhudiwa baadhi ya Makada wakifika katika ofisi za wilaya ya Moshi vijijini kwa lengo la kuchukua fomu hizo.
Miongoni mwa waliorejesha fomu ni pamoja aliyekuwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt Charles Kimei aliyechukua fomu ya kuwania Ubunge katika jimbo la Vunjo ambapo alirejesha fomu yake katika ofisi za CCM wilaya ya Moshi na kupokelewa na katibu wake Miriam Kaaya .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad